Wanafunzi 160 wanusurika kifo baada ya mabweni mawili kuteketea kwa moto Mkoani Arusha.
Zaidi ya wanafunzi mia moja na sitini wa shule ya sekondari Longido wamenusurika kifo baada ya mabweni mawili ya shule hiyo kuteketea kwa moto ikiwa ni shule ya tatu ya serikali mkoa wa Arusha kuungua moto kwa kipindi kisichozidi wiki moja.
ITV ilifika kwenye tukio hilo na kushuhudia moto ukiendelea kuwaka na baadhi ya vifaa vikiteketea kwa moto huku wanafunzi waliyoonekana kufadhaishwa na hali hiyo wakiwa wamesimama nje ya mabweni kisha wakaeleza masikitiko yao kwa matukio ya moto yanayoendelea kwenye shule za sekondari za serikali.
Mkuu wa shule ya sekondari Longido amesema baadhi ya wanafunzi walipata mshituko na kupoteza fahamu lakini wametibiwa na kurudi shuleni bado kuna hitajika juhudi za kuwarudisha kwenye hali ya kawaida kwani sasa hawataki kulala kwenye mabweni kwa hofu ya kupoteza uhai.
Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kuna dalili za hujuma kwenye matukio hayo na kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itahakikisha inakamata wahusika ili kukomesha tabia hiyo.

ZeroDegree.
Wanafunzi 160 wanusurika kifo baada ya mabweni mawili kuteketea kwa moto Mkoani Arusha.
Reviewed by Zero Degree
on
8/07/2016 09:00:00 AM
Rating: