Loading...

Mazoezi ya Polisi Moshi yawatisha wananchi.

Mazoezi ya Polisi mkoani Kilimajaro yaliyodumu kwa takriban saa nne yaliyofanywa na vikosi vya askari wa kutuliza ghasia na magari ya washawasha, yametikisa mji wa Moshi na kuzua hofu kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi walishangazwa na kitendo hicho cha polisi kuzunguka wakiwa na mabomu ya machozi na gari la maji ya washawasha.

Mkazi mmoja, Peter Lyimo alisema ameshtushwa kuona magari ya polisi yakizunguka, huku milio ya milipuko ya mabomu ikisikika.Naye Mary Kavishe alisema: “Tumezoea kuona polisi wakifanya mazoezi kambini kwao, siyo kuzunguka katikati ya mji.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa alisema wanafanya mazoezi ya kawaida ya kujihami na wahalifu na kulinda wananchi na mali zao.

“Ni mazoezi ya kawaida na yanafanyika mkoa mzima kwa ajili ya kuimarisha askari wetu, ili kujihami na matukio mbalimbali ya kihalifu,” alisema.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Mazoezi ya Polisi Moshi yawatisha wananchi. Mazoezi ya Polisi Moshi yawatisha wananchi. Reviewed by Zero Degree on 8/23/2016 11:07:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.