Loading...

Msanii wa Afrika Kusini Leleti Khumalo “Sarafina” hajafariki, taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kifo chake ni za uongo.

Kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikielezea juu ya kifo cha Staa mwenye jina kubwa duniani kutoka Afrika Kusini, Leleti Khumalo ‘Sarafina’ hata hivyo baadhi ya mitandao na magazeti ya Afrika Kusini yamethibitisha kuwa taaifa hizo ni za uongo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Habari wa Afrika Kusini wa Daily Sun, kupitia habari yao iliyochapishwa jana Agosti 13.2016 imekanusha uvumi huo na kuita ni uongo wa kupindukia hivyo watu wenye mapenzi mema na msanii huyo wasitilie manani habari hizo.

Mtandao huo umebainisha kuwa, taarifa za uvumi zilianza kuenezwa kwa mara ya kwanza kupitia mitandao ya kijamii kwa moja ya kurasa za akaunti kutoka Nchini Canada. Hata hivyo kupitia akaunti ya twita ya mtandao wa kijamii wa burudani na mastaa wa Afrika Kusini ambao ni maarufu nchini wa Mzansi ulikanusha uongo huo na kuwatoa hofu wadau na fans wa msanii huyo ambao walipata mshtuko mkubwa waliposikia taarifa hizo.

Msanii huyo, mwaka jana katika mwezi Julai alipata wasaha wa kutembelea Tanzania katika visiwa vya Zanzibar ambapo alikuja kama mgeni maalum wa tamasha la Nchi za Majahazi lijulikanalo kama ZIFF.
Sarafina akiwa katika mkutano na wanahabari Visiwani Zanzibar.





                       


Msanii Leleti Khumalo ‘Sarafina akiwa katika pozi na wanahabari kulia ni Mwanahabari Mwandamizi wa mtandao huu Andrew Chale na Kushoto ni Festo Polea wa gazeti la Mtanzania akifuatiwa na Herieth Makweta Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi. Hii ilikuwa mwaka 2015, wakati wa tamasha la ZIFF.

Credits: DewijBlog
ZeroDegree.
Msanii wa Afrika Kusini Leleti Khumalo “Sarafina” hajafariki, taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kifo chake ni za uongo. Msanii wa Afrika Kusini Leleti Khumalo “Sarafina” hajafariki, taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kifo chake ni za uongo. Reviewed by Zero Degree on 8/14/2016 05:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.