Loading...

VIDEO: Mabingwa wa Ligi kuu ya Uingeleza [ EPL ], Leicester wamponza mtangazaji...aingia Studio akiwa amevaa Boxer.

Gary Lineker ametimiza ahadi yake ya kutangaza Show ya kwanza ya ‘Match of the Day’ ya BBC msimu huu akiwa amevaa chupi ya kiaina tu ‘Bukta’ tu ilikuwa.

Lineker alianza show kwa kuvaa Bukta tofauti na chupi waliyomuandalia.

Wachambuzi wenzake Ian Wright na Alan Shearer walionekana wakicheka nyuma yake wakati akifungua Matangazo.

Gary anatakiwa awaombe radhi mashabiki kwa vile haikuwa Chupi kama alivyoahidi msimu uliopita kwamba, endapo Leicester City wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ya England, angefanya kipindi cha kwanza msimu mpya akiwa amevaa Chupi.

Kwa bahati mbaya kwakwe, Leicester walifanya maajabu na kushinda taji la EPL, hivyo ilimlazimu jana atimize ahadi yake kwenye show ya kwanza ya msimu mpya.


Lineker akiwa kifua wazi aliendelea kujadili na Ian Wright na Alan Shearer wakati wa kipindi hicho.

Lineker akipozi na boxer yake kubwa ya Leicester City wakati wa show ya Match of the Day na alifanya hivyo baada ya mechi ya Manchester City dhidi ya Sunderland kumalizika.

Ahadi ya kutangaza akivalia chupi aliiweke Desemba mwaka jana baada ya Leicester kuichapa 2-1 Chelsea, lakini timu hiyo haikumshawishi mchezaji wake huyo wa zamani kwamba ingetwaa ndoo.

Mapema kabla ya show hiyo, BBC wali-post picha ya nguo za Lineker pamoja na chupi ambayo alitakiwa kuvaa.

Kutazama video hiyo bofya kitufe chekundu hapo chini:


ZeroDegree.
VIDEO: Mabingwa wa Ligi kuu ya Uingeleza [ EPL ], Leicester wamponza mtangazaji...aingia Studio akiwa amevaa Boxer. VIDEO: Mabingwa wa Ligi kuu ya Uingeleza [ EPL ], Leicester wamponza mtangazaji...aingia Studio akiwa amevaa Boxer. Reviewed by Zero Degree on 8/14/2016 04:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.