Loading...

Mbeya City yataja kikosi cha ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom.

kikosi cha mbeya city
MBEYA City imetaja kikosi kamili cha wachezaji 28 iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanne kati yao wakiwa wamepandishwa kutoka timu ya vijana na saba wamejiunga na timu hiyo kutoka klabu nyingine.

Meneja Usajili wa Mbeya City, Frank Mfundo, alisema juzi kuwa nyota wengine watatu kutoka mataifa ya nje watatangazwa mara baada ya taratibu zao za uhamisho kutoka klabu walizokuwa wanazichezea kukamili.

“Hii ni orodha ya wachezaji ambao tayari taratibu zao zimekamilika na ni uhakika kuwa watakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao, hapa majina ya wachezaji ambao tunatarajia kuwasajili kutoka nje ya nchi hatujayajumuisha kwa sababu taratibu zao bado hazijawa sawa.

"Kwa kuwa muda bado upo tunaendelea kulifanyia kazi hilo na imani yetu kubwa tutakamilisha yale machache yaliyobaki ili waweze kujumuika kikosini,” alisema.

Mfundo aliwataja wachezaji hao ambao bado wanasubiri kukamilishwa kwa taratibu zao ili kujumuishwa kikosini kuwa ni Hemedy Murutabose aliyekuwa akichezea Bujumbura City ya Burundi, Sankhani Mkandawile na Owen Chaima waliokuwa wakicheza kwenye kikosi cha Big Bullet ya Malawi.

“Tuko kwenye hatua nzuri, naamini kabla ya muda wa mwisho wa dirisha la usajili kufungwa hapo Septemba 6, mwaka huu tutakuwa tumeshakamilisha kila kitu kuhusu wachezaji hao ambao walikuwa wamependekezwa na kocha wetu Kinnah Phiri,” alisema.

Wachezaji saba wapya walio kwenye kikosi cha City ni pamoja na Fikirini Bakari na Ayoub Semtawa kutoka Coastal Union, Rajabu Isihaka na Omary Ramadhan ‘Barbatov’ waliotokea African Sports zote za Tanga, Rajabu Zahir aliyetokea Yanga SC, Mohamed Mkopi kutoka Prisons na Mark Frank Makolo aliyetokea Azam FC.

Kwa upande wa wachezaji waliopandishwa kutoka timu ya vijana wapo Kenneth Kunambi, Michael Kerenge, Joshua Ibrahim na Peter Mwangosi.

Kikosi kamili cha Mbeya City ni; Juma Kaseja, Fikirini Bakari, Hamis Msabila, John Jerome, John Kabanda, Haruna Shamte, Hassan Mwasapile, Mark Franco Makolo, Tumba Sued, Peter Michael Mwangosi, Rajab Mohamed, Kenny Mwambungu, Medson Mwakatundu, Hamidu Mohamed na Ramadhan Chombo.

Wengine ni Rafael Daud, Ayoub Semtawa ,Joseph Mahundi, Ditram Nchimbi, Joshua Ibrahimu, Omary Ramadhan,Issah Nelson,Michael Kerenge, Mohamed Mkopi, Salvatory Nkulula, RajabuAbdallah, Geofrey Mlawa na Kenneth Kunambi. City itaanza na Kagera Sugar katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage Shinyanga Agosti 20, mwaka huu.


Credits: IPPMedia
ZeroDegree.
Mbeya City yataja kikosi cha ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom.  Mbeya City yataja kikosi cha ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom. Reviewed by Zero Degree on 8/14/2016 04:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.