Loading...

Ndoto za Yanga kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho zayeyuka.

Hesabu za Yanga kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, zimefutika baada ya Medeama ya Ghana kuilaza TP Mazembe ya DR Congo mabao 3-2 katika mchezo mkali wa michuano hiyo uliofanyika mjini Accra, Ghana.

Yanga iliyoilaza MO Bejaia bao 1-0 juzi kwenye Uwanja wa Taifa, ilikuwa ikiomba dua TP Mazembe iifunge Medeama ili kuweka hai matumaini yake, lakini imekuwa kinyume chake.

Mpaka sasa, Yanga ina pointi nne, na ilikuwa ikiombea matokeo hayo huku ikiipigia chapuo TP Mazembe kushinda mchezo wa mwisho utakaopigwa siku 10 zijazo mjini Lubumbashi.

Kwa matokeo hayo, Medeama imefikisha ponti nane ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga na sasa inaacha ushindani kubakia kati ya timu hiyo ya Ghana na MO Bejaia. Mchezo wa mwisho wa timu hizo, unaweza kuwa mgumu au mwepesi kwa timu zote, Medeama inahitaji sare wakati MO Bejaia inahitaji ushindi lakini ili ifuzu, inatakiwa iifunge Medeama mabao 3-0 kwa kuwa Medeama ina wastani mzuri wa mabao.

Ukiangalia mabao ya kufunga na kufungwa, Medeama imefunga mabao nane lakini imefungwa mabao saba wakati MO Bejaia imefungwa mabao mawili yenyewe ikiwa na bao moja la kufunga.

Dalili za Medeama kushinda mchezo huo zilionekana tangu kuanza mchezo huo, ilipata bao la kuongoza dakika ya 32 lililofungwa na Atta Agyei kabla ya Serbong M kuongeza dakika ya 59.

Bolengj aliifungia TP Mazembe bao dakika ya 61 kabla ya Rainford Kalaba kusawazisha katika dakika ya 71. Bao lililoimaliza TP Mazembe, liliwekwa wavuni na Kwesi dakika za majeruhi.

Akizungumza muda mfupi kabla ya matokeo hayo, Kocha wa Yanga, Hans Pluijm alisema walipanga kucheza na TP Mazembe kwa hesabu ya ushindi na kusisitiza kwamba matokeo

ya aina nyingine tofauti na ushindi hayatakuwa na maana kwao.

“Tulikubaliana na wachezaji wangu tukapambane kufa na kupona katika mchezo huo, kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa maslahi ya Yanga,” alisisitiza Pluijm.


Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Ndoto za Yanga kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho zayeyuka. Ndoto za Yanga kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho zayeyuka. Reviewed by Zero Degree on 8/15/2016 09:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.