Loading...

Utabiri wa Mourinho baada ya Pogba kutua Man U.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anaamini kwamba timu yake itarejesha kiasi cha fedha baada ya kuvunja rekodi ya usajili wa dunia kwa kumsajili Paul Pogba, huku akisisitiza kwamba nyota huyo ana miaka takriban kumi mbele ya kung’aa.





Pogba amekamilisha uhamisho wake wa euro mil 110 kurudi United akitokea kwa kibibi kizee cha Turin Jeventus mapema leo asubuhi.

“Ana nafasi ya kuwa moyoni mwa mashabiki wa klabu hii kwa miaka kumi na zadi,” Mourinho amesema.

“Paul ni moja ya wachezaji bora duniani na atakuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha United na nataka nimfanye awe tegemeo kubwa kwa siku za usoni.”

“Ana kasi, nguvu, anafunga na ana uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo vizuri kuliko wachezaji wengi ambao wamemzidi umri.”

“Kwa umri wake wa miaka 23, ana nafasi ya kujimilikisha nafasi yake kwa miaka mingi zaidi. Bado ni kijana ataendelea kuimarika zaidi.”

Pogba amedumu Juventus kwa miaka minne, ameshinda ubingwa wa Serie A kwa miaka yote minne. Mourinho anaamini Mfaransa huyo atahamishia makali yake kunako Old Trafford na kurejesha heshima ya Man United iliyopotea kwa tangu msimu wa 2012-13.


Credits: ShaffihDauda
ZeroDegree.
Utabiri wa Mourinho baada ya Pogba kutua Man U. Utabiri wa Mourinho baada ya Pogba kutua Man U. Reviewed by Zero Degree on 8/09/2016 07:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.