Loading...

Wapika gongo jijini Mwanza wakiona cha moto.

Mtambo wa kutengenezea gongo.
SERIKALI wilayani Kwimba, imeanza msako mkali dhidi ya watu wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo na kukamata mitambo inayotumika kutengenezea pombe hiyo inayodaiwa kusababisha uharibifu wa mazingira.

Akizungumza katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa wilaya ya hiyo, Mtemi Msafiri, alisema msako huo umeanza kwa kamati ya ulinzi na usalama, wilayani humo kukamata lita 573 za pombe hiyo katika vijiji vitano, mitambo 10 ya kutengenezea pombe hiyo na madumu 11 yenye ujazo wa lita tano na lita 20.

“Msako huu umewezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 38, watuhumiwa 25 kati ya hao wamekuhukumiwa kutokana na kujihusisha na biashara ya upikaji wa pombe hiyo,hii inaonyesha wananchi hawapatiwi elimu ikiwa na kusababishwa na watendaji wa kata wanashirikiana na wapikaji haoharamu, hivyo kwayeyote atakayebainika kushindwa kusimamia suala hili katika kata yake nibora atupishe kabla sheria haijachukua mkondo wake,”alisema.

Aidha,pombe hiyo inayodaiwa kuwa tegemeo kubwa la kiuchumi kwa baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo, hasa kinamama wazee na wanawake wajane katika kujipatia riziki na kipato chao,hivyo serikali itawajibika katika kuwawezesha watu hawa kupitia fedha za mfuko wa asilimia tano ya kinamama na vijana ili waweze kuanzisha shughuli nyingine na siyo ya upikaji wa pombe haramu,”alisema.

Credits: IPPMedia
ZeroDegree.
Wapika gongo jijini Mwanza wakiona cha moto. Wapika gongo jijini Mwanza wakiona cha moto. Reviewed by Zero Degree on 8/26/2016 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.