Loading...

Watanzania washauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili ili kuutangaza utamaduni wa nchi.

Watanzania wameshauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili katika ulimwengu wa uandishi ili kuutangaza Utamaduni wa nchi.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).

Mkurugenzi amesema kuwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na kuenzi juhudi za kuenzi na kuendeleza juhudi za watetezi za masuala ya lugha wa masuala ya Lugha na Utamaduni wa mtanzania.

Ameongeza kuwa Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa imeandaa kanuni za Sheria ya BAKITA ya mwaka 1967 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni ambayo itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili waandishi hapa nchini pamoja na haki zao katika kuendeleza fani mbalimbali za Lugha.

“Katika azma ya kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa Rais wetu Mhe.Dkt John Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika hotuba zake mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat Shani.

Kwa upande wake mmoja ya wajumbe wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa katika risala yao kwa mgeni rasmi amesema kuwa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania(UWARIDI) wameamua kutafuta njia ya kurudisha, kutetea, kulinda na kuipandisha heshima yetu kama waandishi na heshima ya kazi zetu zote.

“Tumeamua kutafuta mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu zinatambuliwa rasmi kiserikali na kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja wetu ambao utakuwa na sauti katika kutetea haki za waandishi na kazi zao alisisitiza Bi. Matilda.

umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) umeanzishwa kwa lengo la kuwatetea waandishi wa Riwaya nchini ili waweze kunufaika na kazi zao.

Credits: DewijBlog
ZeroDegree.
Watanzania washauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili ili kuutangaza utamaduni wa nchi. Watanzania washauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili ili kuutangaza utamaduni wa nchi. Reviewed by Zero Degree on 8/26/2016 11:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.