Loading...

Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini.

Rais Kim Jong-un na mkewe Ri Sol-ju.
 Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.

Tangazo la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya muungano ya Seoul na limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti moja kusema maafisa wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa kulipuliwa kwa makombora ya kutungua ndege.

Gazeti hilo lilisema wawili hao waliuawa mapema mwezi huu.

Waziri huyo wa elimu anadaiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika katika ufisadi baada yake kusinzia katika mkutano wa kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-un.


Waziri huyo alichunguzwa baada ya kusinzia mkutano wa Rais Kim Jong-un.
Mapema mwezi huu, naobu balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza aliikimbia nchi yake na kuhamia rasmi Kusini.

Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini. Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini. Reviewed by Zero Degree on 8/31/2016 08:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.