Loading...

Yanga, Mtibwa Sugar kujipima Jumamosi.

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Yanga wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit.

Mchezo huo ni kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia kutoka Ghana itakayofanyika Agosti 13 mwaka huu na msimu ujao wa Ligi Kuu.

Akizungumza jana jijini, Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema kuwa maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vizuri na klabu zote mbili zimeshathibitisha kucheza mchezo huo.

Deusdedit alisema kuwa uamuzi wa kutafuta mechi hiyo ya kirafiki umetokana na mapendekezo yaliyotolewa na benchi la ufundi ambalo linahitaji kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi iliyopita dhidi ya Medeama FC ya Ghana ambayo walikubali kichapo cha mabao 3-1 na kuwaweka kwenye nafasi ngumu ya kusonga mbele.

"Timu inaendelea vizuri na mazoezi na kutakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mtibwa Sugar. Mchezo huo ni wa kujipima nguvu na utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Agosti 6 saa 10:00 jioni," alisema katibu huyo.

Mbali na kujiandaa na mchezo dhidi ya Mo Bejaia, Yanga pia inajiimarisha kuikabili Azam FC katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii utakaofanyika Agosti 17 kwenye Uwanja wa Taifa na baadaye kuwafuata TP Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

ZeroDegree.
Yanga, Mtibwa Sugar kujipima Jumamosi.  Yanga, Mtibwa Sugar kujipima Jumamosi. Reviewed by Zero Degree on 8/03/2016 09:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.