Loading...

Schweinsteiger atemwa katika kikosi cha United kitakachoshiriki ligi ya EUROPA.

Siku chache baada ya jina lake kujumuishwa kwenye kikosi cha Man United kwenye msimu wa ligi wa 2016-17, Bastian Schweinsteiger ametoneshwa kidonda na kocha wake Mourinho baada ya jina lake kutojumuisha katika kikosi kitakachoshiriki Ligi ya Europa.

Kiungo huyo mkongwe tayari amestaafu soka la kimataifa na Jumatano alifanyiwa sherehe ya kuagwa kwenye Timu ya Taifa ya Ujerumani maarufu kama Die Manschaft kufutiwa kufanyika mchezo maalum dhidi ya Finland na kushinda mabao 2-0.



Schweinsteiger ambaye huko nyuma alicheza kwa mafanikio makubwa kunako klabu ya Bayern Munich ameichezea Ujerumani michezo 121.

Katika kikosi hicho, viungo 10 wametajwa huku jina la Schweisteiger likikosekana.

Majina ya kikosi kizima cha wachezaji 27 wa Manchester United yaliyotajwa:


Golini:
David De Gea, Sergio Romero, Sam Johnstone

Mabeki:
Eric Bailly, Phil Jones, Marcus Rojo, Daley Blind, Chris Smalling, Luke Shaw, Timothy Fosu-Mensah, Antonio Valencia, Matteo Darmian, Axel Tuanzebe

Viungo:
Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Michael Carrick, Ashley Young, Ander Herrera, Henrikh Mkhitaryan, Marouane Fellaini, Morgan Schneiderlin, Memphis Depay

Washambuliaji:
Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial, Marcus Rashford.

Credits: ShaffihDauda
ZeroDegree.
Schweinsteiger atemwa katika kikosi cha United kitakachoshiriki ligi ya EUROPA. Schweinsteiger atemwa katika kikosi cha United kitakachoshiriki ligi ya EUROPA. Reviewed by Zero Degree on 9/04/2016 10:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.