Loading...

Neuer nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani.

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer ametanazwa kuwa ndiye nahodha mpya wa timu ya taifa(Ujeruman), baada ya aliyekuwa na wadhifa huo, Bastian Schweinsteiger kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa.


Bastian Schweinsteiger akitokwa na machozi wakati alipokuwa akiagwa na mashabiki wa timu yake ya taifa ya Ujerumani.
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew alitangaza uamuzi wake wa kumteuwa Neuer siku ya Alhamisi, ikiwa ni siku moja baada ya Schweinsteiger kucheza mechi yake ya mwisho ya kirafiki na timu yake ya taifa ambapo Ujerumani ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Finland.

Neuer 
mwenye umri wa miaka 30 ambaye pia ndiye golikipa klabu ya Bayern Munich, alionekana kwenye kikosi cha Ujerumani kwa mara ya kwanza Juni 2009 na alishinda Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil akiwa na timu yake ya taifa ya Ujerumani. Ameshiriki katika michezo 71 na timu yake ya taifa mechi pia ndiye aliyekuwa kipa bora wa FIFA miaka/misimu mitatu iliyopita.

Loew anasema Neuer ni "mrithi mwenye 
mantiki" kwa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Bastian Schweinsteiger na ataleta "kila kitu ambacho naweza tarajia toka kwa kiongozi."

Golikipa wa Timu ya Taifa ya ujerumani na Klabu ya Bayern Munich, Manuel Neuer.
Kwa upande Mlinda mlango huyo, Manuel Neuer; yeye anasema ni fahari kubwa kwake yeye kuwa nahodha na anafahamu nini maana ya kiongozi, hivyo kuahidi kuwa mfano wa kuigwa.

Credits: NBC Sports
ZeroDegree.
Neuer nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani. Neuer nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani. Reviewed by Zero Degree on 9/02/2016 04:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.