Loading...

Mwenyekiti atuhumiwa kummwagia tindikali katibu.

Polisi mkoani Geita, inamshikilia Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorotoro A, Gervas Kaiyelelo kwa tuhuma za kummwagia tindikali Katibu wa CCM Tawi La Nyantorotoro, Kulwa Kazinga kwa kile kinachodaiwa ni uhasama wa kisiasa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema tukio hilo lilitokea Agosti 31 usiku, wakati katibu huyo akielekea nyumbani kwake. Kapufi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha tukio hilo ni uhasama wa kisiasa baina ya mwenyekiti huyo ambaye ni wa Chadema na katibu wa CCM.

Akizungumza kwa shida kutokana na majeraha aliyoyapata ikiwamo kuungua maeneo ya uso na kifuani, Kazinga alisema siku hiyo akiwa na jirani yake aliyemtaja kwa jina la Selestine Misungwi wakitokea makao makuu ya kata hiyo, alitokea mtu msituni na kummwagia majimaji ambayo yalianza kumuwasha na alihisi maumivu makali.

Source: Mwananchi
Zerodegree.
Mwenyekiti atuhumiwa kummwagia tindikali katibu. Mwenyekiti atuhumiwa kummwagia tindikali katibu. Reviewed by Zero Degree on 9/04/2016 08:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.