Loading...

Bob Bradley kutua Swansea City??

Bob Bradley anaendelea kuhusishwa na ajira za ukocha katika Ligi Kuu ya Uingeleza.
Baada ya kuanza vibaya katika msimu huu, meneja wa sasa wa Swansea City Francesco Guidolinni chini ya shinikizo kubwa litokanalo na ripoti mbali mbali zenye mapendekezo ya kwamba angeweza kupoteza kazi yake na nafasi yake kuchukuliwa na Ryan Giggs.

Hata hivyo, ripoti iliyotolewa na gazeti la Sun inasema kuwa, wamiliki Swansea kutokea nchini Marekani wanataka kuongea na kocha wa sasa wa Le Havre Bradley, mwenye umri wa miaka 58, kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Guidolin kwenye Uwanja wa  The Liberty Stadium.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya wanaume ya Marekani aliachana na kibarua hicho cha kuinoa USMNT 
tangu mwaka 2011. Kutokana na kuichukua timu ya taifa ya Misri ukingoni katika mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia katika mazingira magumu zaidi, yeye huyo huyo akaichukua Stabaek Norway mpaka nafasi ya tatu kwenye ligi kuu na kufuzu mashindano ya Ulaya.

Bradley pia alikuwa nyuma katika malengo yake ya kuipa nafasi Le Havre kupanda na kupata kibali kushiriki Ligue 1 msimu uliopita siku ya mwisho ya mashindano ya mwaka 2015/16, ambapo Le Havre walikoswa koswa kutolewa nje ya ligi daraja la pili Ufaransa.

Pamoja na vijana wa Swans kupoteza pointi sita ndani ya 
michezo yao minne ya Ligi Kuu msimu huu mpaka sasa, ni wazi kuwa mashabiki na pengine bodi ya timu hawana furaha na mwelekeo wa klabu chini ya uongozi wa Guidolin. 

Meneja huyo mkongwe kutokea Italia aliwasili katika nusu ya pili ya msimu uliopita na licha ya kushika kasi vizuri na kuwaweka swansea katika hari nzuri, lakini kupoteza imani kwa nyota wake Ashley Williams na Andre Ayew msimu huu kumekuwa na hali ngumu kwake.

Linapokuja suala la Bradley ripoti inasema kuwa wawekezaji wa Marekani Jason Levien na Steve Kaplan - ambaye kwa sasa ndiye wenyewe sehemu kubwa ya hisa klabuni hapo - wasiwasi wake ni juu ya ukosefu wa uzoefu wa Giggs kama kocha mkuu
 wa timu. Wao wanaamini Bradley atakuwa mgombea kamili wa kujenga mipango endelevu ya kuiletea mafanikio makubwa timu na ni vigumu kupingana na hilo.

Popote Bradley alipokuwa akienda kumefanyika miujiza mingi hususani juu ya bajeti na mara nyingi mbali na matatizo yote aliyoyakuta yeye amefanikiwa kupita matarajio. Swansea ni klabu ambayo si ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika ununuzi wa wachezaji lakini hununua wachezaji wenye umri mdogo na kujipa matumaini makubwa ya kuendeleza vipaji vyao wakati huo huo kuwa na uwezo wa kuiweka timu katika hali nzuri ndani ligi.

Ingawa Giggs bado anaonekana kama mbadal wa Guidolin kama akiodoka Uwanja wa The Liberty Stadium, itakuwa ni vyema kuona kocha Bradley na ujuyi wake anapata kazi anayostahili.

Baada ya kuhusishwa siku za nyuma kupata kazi
 katika vilabu vya West Bromwich albion na vile vile Aston Villa, Hull City, Fulham na isitoshe klabu nyingine kubwa zinazoshiriki ligi kuu, mmarekani huyo toka New Jersey amekuwa hazungumziwi kuhusu uwezo wake na ukitazama mfumo wake kwa ufipi wengi bwanadai hauna tofauti kubwa akina Pep Guardiola na Jurgen Klopp 


"Mimi nitakuambia nini, labda mimi ni mjinga lakini nadhani mimi ni meneja bora na ninaweza fikia katika ngazi hiyo, siwezi kusema ninwapita hao wengine lakina naweza kusema sijpata tu nafasi kama zao." alisema Bradley. Lakini nahisi wale ambao wamecheza chini ya uongoizi wangu wameona uwezo wangu na kuona tofauti zaidi ya waliyokuwanayo awali kuwa kuelekeza ni kazi ngumu na kumekuwa na juhudi kubwa siku zote kuwafanya kuwa bora zaidi. Naimani na kazi nyangu. Mimi sio mtu wa kukaa na laumu laumu bila sababu huwa nafanya juhudi kubwa katika kazi yangu kuwaonyesha watu uwezo wangu na kuona kipi kinatokea."

Labda, Bradley hatimaye atapata kuonyesha nini kikomo cha uwezo wake linapokuja swala la kuinoa timu atapokuja Ligi kuu ya Uingereza.

Source: NBC Sports
ZeroDegree.
Bob Bradley kutua Swansea City?? Bob Bradley kutua Swansea City?? Reviewed by Zero Degree on 9/26/2016 07:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.