Loading...

FIFA imekivunja kikosi kazi cha kuchunguza suala la ubaguzi wa rangi kuelekea Kombe la Dunia nchini Urusi 2018.

MANCHESTER, Uingereza. FIFA imevunja kikosi kazi chake cha kupambana na ubaguzi wa rangi, wakitangaza kukamilika kwa kazi husika licha ya wasiwasi na sintofahamu inayoendelea kuhusu tabia za kibaguzi baada ya Kombe la Dunia kupangwa kufanyikia nchini Urusi mwaka 2018.

FIFA aliwaandikia ujumbe wanachama wa kikosi kazi unaosema kuwa inahakika "kabisa imetimiza shughuli yake hiyo ya muda mfupi" na "inakivunja rasmi kikosi kazi chake na kuwa hakiko katika operesheni hiyo tena."

"Ningeweza ningesema kwamba binafsi nimeshtushwa na uamuzi huo, lakini kwa bahati mbaya mimi si hivyo," mwanachama wa kikosi kazi hicho Osasu Obayiuwana ameliambia shirika moja la habari jana Jumapili. "Tatizo la ubaguzi wa rangi
 linabakia kuwa ni kikwazo kikubwa katika soka, na liko katika hari mbaya sana, ambalo linapaswa kufanyiwa uchunguzi endelevu.

"Mimi binafsi nadhani kwamba kuna mengi zaidi yamebakia ambayo kikosi kazi kingefanya - Mashindano ya Kombe la Dunia la mwaka 2018 yatakayofanyikia nchini Urusi ikiwa ni mmoja wapo. Lakini ni dhahiri kwamba utawala wa FIFA unachukua sura nyingine."


Kikosi kazi kilianzishwa mwaka 2013 na Rais mstaafu wa FIFA Sepp Blatter na kuongozwa na Jeffrey Webb, makamu wa rais wa tume ya utawala ya soka duniani mpaka alipokamatwa mwaka 2015 kufuatia uchunguzi uliofanywa na Shirika la Upelelezi la Marekani akihusiswa na rushwa katika soka.

Webb, ambaye alikiri mashtaka ya kujihusisha katika tuhuma hizo, nafasi yake 
kama mwenyekiti wa kikosi kazi ilichukuliwa mwaka uliopita na rais wa shirikisho la soka Kongo, Constant Omari ambaye pia ni mjumbe wa baraza tawala FIFA.

"Hatukuwahi kuwa na mkutano hata mmoja chini ya uenyekiti wake," alisema Obayiuwana."..nilijaribu kumtumia ujumbe, zaidi ya mara moja, kuuliza ni lini tufanye mkutano. Lakini kamwe sikuwahi kupokea jibu lolote toka kwake. "

Obayiuwana, mwandishi wa habari, mtangazaji na mwanasheria, alipokea barua kutoka FIFA siku ya Ijumaa ikitoa taarifa ya kuvunjwa kwa kikosi kazi.

"Kikosi Kazi cha FIFA dhidi ya unyanyasaji na Ubaguzi kilianzishwa kwa msaada wako kwa misingi ya kufanya kazi kwa muda mfupi ili kuandaa mapendekezo ya FIFA," aliandika Gerd Dembowski, meneja wa idara ya kupambana na ubaguzi FIFA .

"Tunafuraha kuwajulisha kuwa mapendekezo yote ya kikosi kazi yametekelezwa na miradi yote iliyotokana na mapendekezo hayo inaendelea kufanyiwa kazi."

FIFA ilisema kuwa kwa kuanzishwa kwa mfumo wa kupambana na ubaguzi, uzinduzi wa, "Good Practice Guide," kuanziswa kwa timu ya mashujaa katika soka
. Fatma Samoura, mwanamke wa kwanza toka nje ya Ulaya ambaye ni katibu mkuu FIFA , atatoa tuzo hiyo leo SoccerEx Manchester.

FIFA pia aliwaambia wajumbe wa kikosi kazi kwamba mipango yake "kiukweli inazidi mapendekezo ya kikosi kazi hicho" - ikiwa ni pamoja na kuendelea kuipa kipaumbele 
kampeni yao "Sema Hapana kwa ubaguzi wa rangi/Say No To Racism", mikutano ya wanawake katika uongozi na mipango mbali mbali Urusi. Ni chini ya miezi tisa imesalia kwa Urusi kuanza mashindano ya Kombe la Shirikisho, ikiwa ni maandalizi ya Kombe la Dunia la mwaka 2018.

Taarifa iliyotokana na utafiti wa hivi karibuni kutoka SOVA Center(
Moscow) na UEFA-affiliated FARE Network unaonyesha ongezeko la idadi ya maotukio ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa Soka wa Urusi, na kesi nyingi kuisha bila wahusika kupewa adhabu yoyote. Watafiti wametaja matukio 92 ya kibaguzi unaofanywa na mashabiki wa Urusi ndani na karibu na viwanja vya michezo katika msimu wa 2014/15, dhidi ya yale 83 yaa misimu miwili iliyopita.

ZeroDegree.
FIFA imekivunja kikosi kazi cha kuchunguza suala la ubaguzi wa rangi kuelekea Kombe la Dunia nchini Urusi 2018. FIFA imekivunja kikosi kazi cha kuchunguza suala la ubaguzi wa rangi kuelekea Kombe la Dunia nchini Urusi 2018. Reviewed by Zero Degree on 9/26/2016 06:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.