Conte adai Chelsea ni timu kubwa kwenye makaratasi.
Antonio Conte amekiri kuwa Chelsea ni timu kubwa kwenye 'makaratasi' baada ya kuishuhudia ikinyukwa mabao 3-0 na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates Jumamosi iliyopita.
Baada ya mchezo, Conte aliwatupia lawama wachezaji wake kwa kushindwa kufuata maelekezo aliyowapa kabla ya mchezo.
"Nadhani kilichotokea tangu dakika ya kwanza, ni kwamba hatukuwa kwenye kiwango chetu," alisema Conte wakati akizungumza na BT Sport. "Nadhani tulicheza mchezo wa hovyo kabisa dhidi ya timu nzuri, iliyojipanga vizuri.
"Baada ya kipigo, tunafikiria mbele zaidi kurekebisha makosa kwa sababu hadi sasa sisi ni timu kubwa kwenye maandishi."
"Sitaki kuzungumzia makosa, kwa sababu siyo sahihi kufanya hivyo kwa wachezaji," alisema. "Tunaposhinda au kufungwa ni mambo ya kawaida, lakini kubwa ni kufanya kazi kwa bidii. Lakini tufikie malengo na tutaweza kufanya hivyo kwa kurekebisha makosa yetu kwanza."
Kuhusu Eden Hazard na Diego Costa kushindwa kung'ara kwenye mchezo huo, alisema: "Nadhani ni tatizo la jumla la timu na siyo mchezaji mmoja mmoja.
"Kama timu inafanya vizuri, inatoa nafasi kwa kila mchezaji kuonyesha kipaji na uwezo wake. Kama timu haichezi pamoja, ni vigumu sana mchezaji kuweza kuonyesha kipaji na uwezo wake kwenye mechi."
Kipigo hichi kimeifanya Chelsea kuwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya wanaoongoza msimamo Manchester City baada ya mechi sita tu. Hata hivyo, Conte amesema anaangalia namna ya kurekebisha matatizo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kuliko kuangalia mafanikio ya timu nyingine.
"Manchester City wameanza vizuri msimu huu," alisema kocha huyo wa Italia. Kila mtu anawazungumzia, lakini muhimu ni kwamba lazima kwanza umalize matatizo ya nyumbani kwako.
Mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Alexis Sanchez, Theo Walcott na Mesut Ozil yaliipa ushindi wa kwanza Gunners kwenye mechi za Ligi Kuu tangu walipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2011.
Chelsea sasa wako nafasi ya nane kwenye msimamo baada ya kufungwa na Liverpool na Arsenal.
Chelsea sasa wako nafasi ya nane kwenye msimamo baada ya kufungwa na Liverpool na Arsenal.
Baada ya mchezo, Conte aliwatupia lawama wachezaji wake kwa kushindwa kufuata maelekezo aliyowapa kabla ya mchezo.
"Nadhani kilichotokea tangu dakika ya kwanza, ni kwamba hatukuwa kwenye kiwango chetu," alisema Conte wakati akizungumza na BT Sport. "Nadhani tulicheza mchezo wa hovyo kabisa dhidi ya timu nzuri, iliyojipanga vizuri.
"Baada ya kipigo, tunafikiria mbele zaidi kurekebisha makosa kwa sababu hadi sasa sisi ni timu kubwa kwenye maandishi."
"Sitaki kuzungumzia makosa, kwa sababu siyo sahihi kufanya hivyo kwa wachezaji," alisema. "Tunaposhinda au kufungwa ni mambo ya kawaida, lakini kubwa ni kufanya kazi kwa bidii. Lakini tufikie malengo na tutaweza kufanya hivyo kwa kurekebisha makosa yetu kwanza."
Kuhusu Eden Hazard na Diego Costa kushindwa kung'ara kwenye mchezo huo, alisema: "Nadhani ni tatizo la jumla la timu na siyo mchezaji mmoja mmoja.
"Kama timu inafanya vizuri, inatoa nafasi kwa kila mchezaji kuonyesha kipaji na uwezo wake. Kama timu haichezi pamoja, ni vigumu sana mchezaji kuweza kuonyesha kipaji na uwezo wake kwenye mechi."
Kipigo hichi kimeifanya Chelsea kuwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya wanaoongoza msimamo Manchester City baada ya mechi sita tu. Hata hivyo, Conte amesema anaangalia namna ya kurekebisha matatizo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kuliko kuangalia mafanikio ya timu nyingine.
"Manchester City wameanza vizuri msimu huu," alisema kocha huyo wa Italia. Kila mtu anawazungumzia, lakini muhimu ni kwamba lazima kwanza umalize matatizo ya nyumbani kwako.
ZeroDegree.
Conte adai Chelsea ni timu kubwa kwenye makaratasi.
Reviewed by Zero Degree
on
9/26/2016 09:57:00 AM
Rating: