Loading...

Kupatwa kwa Yanga Shinyanga.

HABARI kubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara ni kipigo cha bao 1-0 ilichopata Yanga kutoka kwa Stand United katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga jana Mashabiki wa Simba ambao ni watani wa jadi wa Yanga, wamekuwa wakiliita tukio hilo kwa utani kuwa ni kupatwa kwa Yanga na limechukua sehemu kubwa katika mitandao ya kijamii baada ya mchezo huo kumalizika.

Septemba mosi mwaka huu kulikuwa na tukio kubwa la kupatwa kwa jua kulikotokea Rujewa mkoani Mbeya ambapo watalii kutoka nje ya nchi waliungana na wenyeji kulishuhudia.

Yanga ni bingwa mtetezi wa ligi hiyo na hicho ni kipigo chake cha kwanza katika ligi hiyo inayoshirikisha timu 16, pia alikuwa mwakilishi wa mwisho wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa baada ya timu zingine kutolewa mapema.

Katika mchezo wa jana, Pastor Athanas ndiye aliyewalaza mapema mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wengi.

Mchezaji huyo alifunga bao hilo baada ya pasi safi kutoka kwa mchezaji mwenzake Kelvin Sabato aliyemtoka beki wa Yanga, Vicent Bossou.

Baada ya kumtoka beki huyo alikimbia kwa kasi na kisha kumpangua kipa wa Yanga Ally Mustapha `Barthez’ na kisha kuachia shuti kali lililomwacha kipa huyo akiwa chini. Stand United ilicheza mchezo huo huku ikiwa inashangiliwa mwanzo mwisho wa mchezo na mashabiki wao ambao walikuwa wameujaza uwanja huo.

Kwa ushindi huo, Stand United imefikisha pointi 12 na kupanda kutoka nafasi ya nne hadi ya pili nyuma ya Simba inayoshikilia uongozi ikiwa na pointi 16, huku Yanga ikishuka hadi nafasi ya tatu kutoka ya pili na kubaki na pointi zake 10.

Yanga yenyewe inaendelea kubakia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 10 sawa na Mtibwa Sugar, lakini zikitofautiana kwa uwiano wa mabao.

Stand United: Frank Muhongwe, Revocatus Richard, Abeyiun Saleh, Erick Mrisho, Ebrahm Job, Jacob Masawe, Pastory Atanas, Jeremiah Katula, Kelvin Sabato, Selemani Kassim na Adam Kingwande

Yanga: Ally Mustapha, Juma Abdul, Bin Azi, Andrew Vicent, Mbuyu Twite, Vicent Bossou, Saimon Msuva, Thaban Kamusoko, Khamis Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke.

ZeroDegree.
Kupatwa kwa Yanga Shinyanga. Kupatwa kwa Yanga Shinyanga. Reviewed by Zero Degree on 9/26/2016 09:53:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.