Loading...

Jiko la mkaa lasababisha vifo vya watu watatu wa Familia moja.

WATU watatu wa familia moja wamefariki dunia, huku mmoja akikimbizwa hospitalini, katika kijiji cha Lualaje, kata ya Kipembawe, wilayani Chunya, kutokana na kukosa hewa ya Oxygen baada ya kulala ndani huku wakiwa wameacha jiko la mkaa likiwaka.

Akitoa taarifa ya tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa, aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni baba wa familia hiyo, Leonard Mwashambwa (42) na watoto wake wawili ambao ni Mponeje Leonard mwenye umri wa miaka mitatu na Zaituni Leonard wa mwaka mmoja.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa.
Alisema mama wa familia, Rhoda Darama (22) alikutwa amepoteza fahamu na kwamba alikimbizwa katika hospitali ya wilaya hiyo, ambako alipatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Tukio hilo lilibainika baada ya majirani wa marehemu kuamka asubuhi na kuona milango ya nyumba hiyo haifunguliwi na kuamua kuita kwa ajili ya kuwajulia hali majirani zao hao lakini bila mafanikio.

ZeroDegree.

Jiko la mkaa lasababisha vifo vya watu watatu wa Familia moja. Jiko la mkaa lasababisha vifo vya watu watatu wa Familia moja. Reviewed by Zero Degree on 9/12/2016 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.