Loading...

VIDEO: Baloteli aanza kuwalipa fadhila wafaransa.

Ni watu wachache sana ambao wamewahi kuhofia uwezo wa Mario Balotelli katika kipindi chote tangu kuoneka kwake uwanjani kwa mara ya kwanza, lakini zaidi ni swala la uwezo wake yeye kua makini uwanjani.

Mshambuliaji huyo asiyeisha vituko uwanjani, raia wa Italia inaonekana kuwa anafiti vizuri katika klabu yake mpya ya nchini Ufaransa, Ingawa ndo mwanzoni mwa ligi. Angalau kidogo kwa mchango wake aliouonyesha katika mechi aliyoshiriki wikendi iliyoisha.

Balotelli alifunga mabao mawili siku ya Jumapili wakati timu yake ikitoka kifua mbele baada ya kuichakaza klabu ya 
Marseille goli 3 - 2, na kuipa timu yake ya Nice ishara chanya ya kuendelea kusonga mbele endapo kama mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ataendeleza makali hayo katika msimu huu wa 2016/17.

Nyota huyo
 wa zamani wa klabu ya Liverpool, aliwapa Nice goli la kuongoza baada ya dakika saba za mchezo kuanza kwa kutupia penati. Balotelli alitupia goli jingine la pili katika dakika ya 78 ya kipindi cha pili, kabla ya Wylan Cyprien kufunga bao la ushindi.


ZeroDegree.
VIDEO: Baloteli aanza kuwalipa fadhila wafaransa. VIDEO: Baloteli aanza kuwalipa fadhila wafaransa. Reviewed by Zero Degree on 9/12/2016 12:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.