Loading...

PICHA: Mh. Nape Nnauye alivozindua mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar.

Jumamosi ya Septemba, 11 imeingia katika historia ya soka nchini baada ya ya Waziri wa Michezo, Nape Nnauye kufanya uzinduzi wa mageti ambayo yanatumia mfumo wa tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa.

Shuka chini zaidi kutazama picha za tukio la uzinduzi wa mageti hayo yaliyo katika uwanja wa taifa Jijini Dar.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara yake Prof Elisante Ole Gabriel mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiweka kadi katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki tayari kuingia katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipita katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata utepe kuashiria kuanza kutumika rasmi kwa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watendaji wa Wizara yake, wadau wa michezo, wanamichezo na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa na kuzindua rasmi mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumzia mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa salamu za wadau wa mchezo wa mpira wa miguu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki kwa Serikali katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Mshauri wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki Mhandisi Aloyce Mushi akieleza changamoto mbalilmbali kuhusu mradi huo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai akizungumzia utekelezaji wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki uliotekelezwa na kampuni yake kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai wakitia saini hati za makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika Septemba 11, 2016 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai wakionesha hati za makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika Septemba 11, 2016 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
ZeroDegree.

PICHA: Mh. Nape Nnauye alivozindua mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar. PICHA: Mh. Nape Nnauye alivozindua mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar. Reviewed by Zero Degree on 9/12/2016 10:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.