Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Septemba 14, ..Leicester yaanza vyema kwa kuiadhibu Club Brugge goli 3 - 0.
Frikiki ya Riyad Mahrez iliyopatikana baada ya Vardy kuangushwa akijibu shambulizi. |
Albrighton alifunga bao la kwanza ambapo ilikua ni mara ya kwanza kwa Leicester kushambulia baada ya makosa yaliyofanywa na beki wa kulia wa Club Brugge Luis Hernandez.
Mahrez baadaye alifunga goli la pili, kabla ya kufunga goli la tatu kwa mkwaju wa penalti baada ya Jamie Vardy kuangushwa na kipa wa Brugge.
Jose Izquierdo wa Club Brugge alipata nafasi nzuri lakini akagongesha mpira wake kwenye mlingoti wa goli.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza walionekana kucheza kwa ukomavu mkubwa na kuonyesha wana uwezo wa kushindana katika soka ya Ulaya.
Hiyo ilikuwa mechi yao ya tisa kucheza Ulaya katika historia yao. Aidha, ilikuwa mechi yao ya kwanza kushinda Ulaya tangu ushindi wao dhidi ya Glenavon ya Ireland Kaskazini hatua ya kufuzu kabla ya hatua ya makundi katika Kombe la Wasindi 1961-62, kipa mshindi wa Kombe la Dunia la mwaka 1966 Gordon Banks alipokuwa mlinda lango wao.
Mashabiki wa Leicester walitengewa tiketi 1,400 pekee mechi hiyo. |
Winga wa Algeria Riyadh Mahrez alifunga mabao mawili.
Leicester watarejea uwanjani katika Ligi kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi watakapokuwa wenyeji wa Burnley saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki. Mechi yao nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa Jumanne ya Tar 27 Septemba, watakapokuwa wenyeji wa FC Porto.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa zilizochezwa jana Tar 14, Septemba:
- Bayern 04 Leverkusen 2 - 2 CSKA Moscow
- FC Porto 1 -1 F.C. Copenhagen
- Juventus 0 - 0 Sevilla
- Lyon 3 - 0 Dinamo Zagreb
- Legia 0 - 6 Dortmund
- Lyon 3 - 0 D. Zagreb
- Manchester City 4 - 0 B. Monchengladbach
- Real Madrid 2 - 1 Sporting
- Tottenham 1 - 2 Monaco
ZeroDegree.
Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Septemba 14, ..Leicester yaanza vyema kwa kuiadhibu Club Brugge goli 3 - 0.
Reviewed by Zero Degree
on
9/15/2016 11:05:00 AM
Rating: