Baada ya PIZA, ..Guardiola apiga marufuku wachezaji wake kutumia internet.
Mhispania huyo ameandaa baadhi ya maeneo ya Academy za Man City kwa ajili ya kufanyia mazoezi ambako hakuna 3G wala mfumo wa Wi-Fi ndani yake.
Pablo Zabaleta amebainisha hoja moja ya kuwa, lengo la kufanya hivyo ni kuepusha wachezaji kutoathiriwa kisaikolojia na simu zao au vifaa vingine vya muziki.
"Anatulazimisha kuwa na kifungua kinywa na pia chakula cha mchana pamoja katika klabu hiyo. Katuweka kizuizini. Hatuwezi hata kutumia 3G," beki huyo aliiambia TYC Sportsv ya Argentina.
Zabaleta, ambaye anafurahia kucheza chini ya Guardiola kwa kupata nafasi na muda wa kutosha uwanjani, ni mmoja wa wachezaji wanaofit katika mbinu za kocha huyo mwenye umri wa miaka 45. "Siku zote mchezaji unataka na unakua na ndoto ya kufundishwa na makocha bora, na leo mimi nina nafasi ya kufanya kazi na kocha bora," alisema. "Kwa kweli, unajifunza mambo mengi, hasa njia wewe kuishi kiuchezaji. Na zaidi ya elimu, ni mapenzi yake ya soka . "
Mabadiliko mengine yaliyotolewa na Guardiola ni pamoja na kupiga marufuku wachezaji wake kula pizza baada ya mechi, na kwa sasa wachezaji wanakula karanga za kutosha. Guardiola pia ametoa maelekezo kwa kikosi chake kula pamoja kwenye Uwanja wa Etihad kuelekea michezo ya nyumbani.
Wachezaji tena hawana haja ya kukaa CFA kabla ya mechi za nyumbani na kama ukibainika kuongezeka uzito sana unajiweka katika hatari ya kufanya kazi mbali na kikosi cha kwanza, kama ilivokuwa kwa Samir kabla ya msimu.
ZeroDegree.
Baada ya PIZA, ..Guardiola apiga marufuku wachezaji wake kutumia internet.
Reviewed by Zero Degree
on
10/05/2016 02:14:00 PM
Rating: