Loading...

Chura wa Snura kuanza kuruka upya tena.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imemruhusu msanii Snura Mushi maarufu kama Snura kutoa wimbo wake wa chura kwenye luninga ukiwa na muonekano mpya wenye maadili na redioni pia kupigwa.

Hayo yamesemwa na Msanii huyo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo na kusema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kukata rufaa na kuomba radhi wizarani.

Msanii Snura Mushi.
"Barua yangu imejibiwa na nimeruhusiwa kucheza wimbo wa chura ila upo katika maadili zaidi, ni kweli ule wa mwanzo haukuwa na maadili," amesema Snura


ZeroDegree.
Chura wa Snura kuanza kuruka upya tena. Chura wa Snura kuanza kuruka upya tena. Reviewed by Zero Degree on 10/05/2016 02:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.