Benki bubu zapigwa ‘STOP’.
MKUU wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo. |
Mwaipopo alitoa amri hiyo juzi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Alisema kuna baadhi ya vikundi ambavyo havijasajiliwa kisheria vimekuwa vikitoa mikopo, jambo ambalo limekuwa likisababisha wananchi kutozwa riba kubwa huku wengine wakifilisiwa mali zao.
Kutokana na hali hiyo, Mwaipopo alisisitiza kwamba kuanzia sasa ni marufuku kwa kikundi au vikundi kufanya shughuli za utoaji wa mikopo ya fedha kwa wananchi, iwapo vitajitambua kwamba havina usajili wowote unaotambulika kisheria.
Alisema kikundi chochote kitakachothubutu kukiuka agizo hilo, hatua kali na za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia kikao hicho pia kuwaagiza wenyeviti wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu upandaji wa miti katika maeneo yao.
Alisema wilaya ya Igunga inaongoza kwa uharibifu wa mazingira kutokana na kukata miti ovyo pasipo kufuata utaratibu, huku akidai kwamba serikali haitakuwa tayari kuona misitu ikikatwa huku upandaji wa miti hiyo kutofanyika.
Aidha, aliwaagiza pia watendaji wa vijiji na kata kuwasomea wananchi mapato na matumizi pamoja na kuwashirikisha katika kuchangia maendeleo badala ya kutegemea kila kitu kitolewa na serikali.
Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa wanaounda Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga, Abel Shampinga, Joseph Michaeli na Saidi Makei, kwa nyakati tofauti waliiomba serikali kudhibiti mifugo inayozurura ovyo ili kunusuru miti itakayopandwa na wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga, Pascrates Kweyamba, aliwataka wenyeviti wa serikali za mitaa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria pasipo kuingiza siasa ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato ili kuiwezesha mamlaka hiyo kujiendesha.
ZeroDegree.

Reviewed by Zero Degree
on
10/29/2016 12:51:00 PM
Rating: