Loading...

Mourinho aendeleza lawama kwa wachezaji wake, safari hii ni zamu ya Pogba.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amemkosoa Paul Pogba kutokana na kiwango chake cha chini alichoonesha kwenye mchezo wa jana dhidi ya Liverpool ulioisha kwa suluhu.

Wakati United walionekana kucheza vizuri zaidi katika safu yao ya ulinzi na kuwapa Liverpool wakati mgumu kupenya, lakini safu yao ya ushambuliaji ilionekana kuwa likizo.

Kufuatia hali hiyo Mourinho ameonekana kutupa lawama zake kwa Pogba kwa kutocheza vizuri pamoja na Zlatan Ibrahimovic ambaye alikosa nafasi moja ya wazi.




“Kama tungepata goli moja, basi tungekuwa tumemaliza kila kitu,” Mourinho alisema na kuongeza: “Sielewi Pogba alikuwa wapi, nilitegemea pasi nyingi za mpenyezo (penetration passes) kutoka kwake.

“Kwa upande wa safu ya ulinzi tulikuwa bora sana, ila tulipaswa kufanya kitu kingine cha ziada. Tulipata nafasi moja adhimu sana ambayo nilidhani Zlatan angemaliza mchezo lakini haikuwa hivyo.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu kwetu na kwao pia. Ulikuwa mgumu zaidi kwao kuliko kwetu. Tulianza vyema na tuliwadhibiti kwa kiasi kikubwa.

“Mchezo ulikuwa mikononi mwetu. Tuliudhibiti kwa kiasi kikubwa. Tungeweza kushawashi mashabiki zaidi ya pale. Walikuwa na fikra kwamba mchezo ungekuwa rahisi sana.”

Mchezo unaofuata United watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Fenerbahce, mchezo wa Europa League utakaochezwa Alhamisi wiki hii katika Uwanja wa Old Trafford.


ZeroDegree.
Mourinho aendeleza lawama kwa wachezaji wake, safari hii ni zamu ya Pogba. Mourinho aendeleza lawama kwa wachezaji wake, safari hii ni zamu ya Pogba. Reviewed by Zero Degree on 10/18/2016 11:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.