Loading...

Mshike mshike ligi kuu ya Uingereza kuendelea tena kesho Jumamosi Tar 15, Octoba.

Ligi kuu ya England inaendelea tena wikiendi hii kwa michezo saba kucheza baada kusimama kupisha michezo ya kimataifa.

Wachezaji wa Leicester City.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Leicester City, watakua ugenini Stamford Bridge, kuwakabali wenyeji Chelsea. Washika bunduki wa London Arsenal wao watakua nyumbani katika dimba la Emirate kuwalika Swansea City.

Matajiri wa jiji la Manchester Man City, watawakaribisha Everton mchezo utakaopigwa katika dimba la Etihad, Fc Bournemouth wao watakipiga na Hull city.

Stoke City watakua nyumbani katika dimba la Britania kucheza na Paka Weusi wa Sunderland, West Bromwich Albion watapimana ubavu na Tottenham.

Wachezaji wa wagonga nyundo wa London West Ham United.

Wagonga nyundo wa London West Ham United watakua na kibarua pevu kwa kupepetana na Tai wa Crystal Palace.


ZeroDegree.
Mshike mshike ligi kuu ya Uingereza kuendelea tena kesho Jumamosi Tar 15, Octoba. Mshike mshike ligi kuu ya Uingereza kuendelea tena kesho Jumamosi Tar 15, Octoba. Reviewed by Zero Degree on 10/14/2016 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.