Loading...

Mwalimu asakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa kidato cha nne.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa.
Polisi mkoani Kilimanjaro inamsaka mwalimu wa Shule ya Sekondari Lemira wilayani Hai, anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne na kukimbilia kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa mzazi wa mwanafuzi huyo na mkuu wa shule wanashikiliwa ili kusaidia kupatikana kwa mwalimu huyo.

Amesema mzazi aligundua kuwa mwanaye ana ujauzito wa miezi mitano na alipomuuliza alimwambia mhusika ni mwalimu wake. “Mzazi wa mtoto alimfuata mwalimu huyo aliyekubali kuwa ujauzito ni wake na kwamba atamuoa. Alimtaka aweke kwenye maandishi kuwa ujauzito ni wake na atamuoa,” alisema Mutafungwa.

Amesema mwalimu huyo alikubali na kuandika kuwa atamuoa mwanafuzi atakapojifungua na kwamba, mkuu wa wilaya alipopata habari hizo alizifuatilia ili kujua sababu.

Alisema alipoitwa kwa mkuu wa wilaya, mwalimu huyo alikimbia hivyo kusababisha kukamatwa mzazi wa mtoto na mkuu wa shule ili kusaidia kupatikana kwake.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa amewataka walimu kuacha kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi na atakayebainika sheria kali zitachukuliwa.

ZeroDegree.
Mwalimu asakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa kidato cha nne. Mwalimu asakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa kidato cha nne. Reviewed by Zero Degree on 10/14/2016 09:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.