Simba watoa kejeli ya mwaka.
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, leo watashuka dimbani kupambana na Mwadui FC kwenye mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage, mkoani Shinyanga, huku Wekundu wa Msimbazi hao wakitamba kuendeleza moto wao kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 kwa madai kuwa hakuna timu yoyote inayowatisha msimu huu.
Simba mpaka sasa wamecheza michezo 11 na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa pointi 29 na kuwazidi kwa pointi tano watani wao wa jadi, Yanga wenye pointi 24, huku wakiwa wamecheza idadi sawa ya mechi.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema lengo lao ni kutwaa ubingwa msimu huu hivyo kila mechi kwao ni fainali.
“Timu inafanya vizuri kwa sasa na lengo ni kutwaa ubingwa hivyo kila mechi kwetu ni fainali, tunaamini tutafanya vema kwenye mchezo huu kikubwa tunaomba dua tu,” alisema.
Hata hivyo, Simba haijawahi kuifunga Mwadui iliyokuwa ikinolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye kwa sasa amejiuzulu toka timu hiyo imepanda daraja Februari 2015.
Mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo ulichezwa Desemba 15 na mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliochezwa Mwadui Complex.
Mechi ya marudiano ilifanyika Mei 8, 2016 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee lililofungwa na mshambuliaji, Jamal Mnyate ambaye kwa sasa yupo Simba liliwapa Mwadui ushindi wa bao 1-0.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 11, wakati Mwadui FC ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 13.
Safu ya ulinzi ya Mwadui imeruhusu mabao 10 na ile ya ushambuliaji imefunga mabao tisa tu. Simba kwa upande wao wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 21 na kuruhusu mabao matatu katika nyavu zao.
Katika hatua nyingine, mechi nyingine za leo ni Mbeya City dhidi ya Majimaji itakayochezwa Uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya, JKT Ruvu dhidi ya Ndanda na Toto Africans akiwakaribisha Mtibwa Sugar.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Simba watoa kejeli ya mwaka.
Reviewed by Zero Degree
on
10/29/2016 11:39:00 AM
Rating: