Loading...

TFF yaiadhibu Simba kwa uharibifu wa viti vya uwanja wa taifa, ..mwamuzi Martin Saanya anachunguzwa [ Taarifa maalum toka TFF iko hapa ].

Kamati ya bodi uendeshaji wa ligi imetoa adhabu kwa vilabu kadhaa kufutia vilabu hivyo kukutwa na makosa mbalimbali.

Kubwa zaidi na lililokuwa likisubiriwa ni kuona hatua gani zitachukuliwa kwa klabu ya Simba kufuatia mashabiki wake kung’oa viti  na la refa Martin Saanya kukubali goli la Amissi Tambwe aliyekuwa amehushika mpira wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga uliochewa October Mosi kwenye uwanja wa taifa.

TFF imetoa adhabu kadhaa kuhusiana na matukio mbalimbali sambamba na kuipiga faini Azam FC kwa kucheza mechi ikiwa imevaa jezi zenye logo ya mdhamini upande mmoja, hata hivyo refa aliyefungiwa ni Ahmed Seif kwa kushindwa kumudu mechi ya African Lyon na Mbao FC, hivyo amefungiwa miezi sita.

Kwa upande wa Martin Saanya TFF imetangaza kuwa imefuta kadi nyekundu aliyomuonesha Jonas Mkude wakati wa mechi ya Yanga na Simba, lakini refa huyo anachunguzwa kufuatia uchezeshaji wake aliouonesha katika mechi hiyo.


Simba imetozwa faini ya shilingi 5,000,000 (milioni tano) pamoja na kulipa gharama za uharibifu wa viti uliofanywa na mashabiki wa klabu hiyo.

Soma taarifa rasmi iliyotolewa na TFF kuhusu adhabu mbalimbali zilizotolewa kwa vilabu vilivyokutwa na hatia katia makosa ambayo vilikuwa vikituhumiwa nayo.



ZeroDegree.
TFF yaiadhibu Simba kwa uharibifu wa viti vya uwanja wa taifa, ..mwamuzi Martin Saanya anachunguzwa [ Taarifa maalum toka TFF iko hapa ]. TFF yaiadhibu Simba kwa uharibifu wa viti vya uwanja wa taifa, ..mwamuzi Martin Saanya anachunguzwa [ Taarifa maalum toka TFF iko hapa ]. Reviewed by Zero Degree on 10/05/2016 05:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.