Loading...

Anayetuhumiwa kutoboa watu macho apandishwa kizimbani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimkabidhi Said Ally msaada wa Sh500,000 ili zimsaidie baada ya kutobolewa macho na mtu anayesadikiwa mwizi katika eneo la Buguruni karibu na kituo cha mafuta. Makonda alimtembelea kijana huyo nyumbani kwake Mabibo Hostel juzi.
Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama Scorpion amepandishwa kizimbani na katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kusomewa tena shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha.


Scorpion ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Ally, mkazi wa Mabibo Hostel, alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Septemba 23, mwaka huu.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Adolf Sachore leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka umeieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.



ZeroDegree.
Anayetuhumiwa kutoboa watu macho apandishwa kizimbani. Anayetuhumiwa kutoboa watu macho apandishwa kizimbani. Reviewed by Zero Degree on 10/05/2016 05:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.