VIDEO: Barcelona walivyomdhalilisha kocha wao wa zamani, Pep Guardiola kwa kichapo cha bao 4 - 0.
Michuano ya klabu bingwa ulaya imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick.
![]() |
Messi amefunga magoli 10 katika michezo nane ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya. |
Barcelona nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu.
![]() |
Bravo atakosa mchezo wa maruduiano Novemba 1. |
Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn.
![]() |
Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi mnono. |
Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jana.
- Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven
- Paris Saint-Germain 3-0 Basel
- Dynamo Kiev 0-2 Benfica
- Napoli 2-3 Besiktas
- FC Rostov 0-1 Atlético Madrid
- Arsenal 6-0 Ludogorets
- Celtic 0-1 B. Monchengladbach
ZeroDegree.
VIDEO: Barcelona walivyomdhalilisha kocha wao wa zamani, Pep Guardiola kwa kichapo cha bao 4 - 0.
Reviewed by Zero Degree
on
10/20/2016 09:49:00 AM
Rating:
