Loading...

VIDEO: Mashabiki wa Coastal Union walivyompiga mwamuzi.

Mwamuzi Thomas Mkombozi kutoka Kilimanjaro alishambuliwa na mashabiki wa Coastal Union kwa kile kilichotafsiriwa ni maamuzi yenye utata aliyokuwa akitoa wakati wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya KMC.

Varangati kubwa liliibuka baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambapo polisi ilibidi kumsaidia mwamuzi kumpeleka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kumnusuru na kipigo toka kwa mashabiki.

Mchezo huo ulimalizika kwa kwa KMC kuibuka mshindi baada ya kuifunga Coastal kwa magoli 3-2. KMC walifunga magoli yao kupitia kwa Augustino Samson aliyefunga magoli mawili huku goli la tatu likifungwa na Rashid Rosha huku magoli ya Coastal yakifungwa na Bakari Nondo na Emanuel Mbaga.



ZeroDegree.
VIDEO: Mashabiki wa Coastal Union walivyompiga mwamuzi. VIDEO: Mashabiki wa Coastal Union walivyompiga mwamuzi. Reviewed by Zero Degree on 10/17/2016 11:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.