Yanga waitisha mkutano wa Dharura.
KLABU ya Yanga imeitisha Mkutano Mkuu wa Dharura ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 23, mwaka huu, huku ajenda wala eneo ambalo mkutano huo utafanyika likiwa halijawekwa wazi.
“Klabu ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama wote wa Yanga kuwa Oktoba 23, mwaka huu, kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Dharura, tunaomba wanachama wote wafike bila kukosa,” alisema Baraka.
Baraka alisema mkutano ni muhimu, hivyo wanachama wote wanaoitakia mema klabu hiyo ni vyema wakafika ili kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi mapana kwa timu yao.
Pamoja na Baraka kushindwa kuweka wazi ajenda za mkutano huo, lakini kuna taarifa kuwa moja ya ajenda itakayojadiliwa katika mkutano huo ni kuwapa wanachama tafsiri ya mkataba wa kuikodisha nembo ya timu hiyo kwa miaka 10, ambao klabu hiyo imeingia na Kampuni ya Yanga Yetu Limited.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema siku chache kabla ya mkutano huo, wanachama watajulishwa juu ya ajenda na sehemu ambayo unatarajiwa kufanyika.
“Klabu ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama wote wa Yanga kuwa Oktoba 23, mwaka huu, kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Dharura, tunaomba wanachama wote wafike bila kukosa,” alisema Baraka.
Baraka alisema mkutano ni muhimu, hivyo wanachama wote wanaoitakia mema klabu hiyo ni vyema wakafika ili kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi mapana kwa timu yao.
Pamoja na Baraka kushindwa kuweka wazi ajenda za mkutano huo, lakini kuna taarifa kuwa moja ya ajenda itakayojadiliwa katika mkutano huo ni kuwapa wanachama tafsiri ya mkataba wa kuikodisha nembo ya timu hiyo kwa miaka 10, ambao klabu hiyo imeingia na Kampuni ya Yanga Yetu Limited.
ZeroDegree.
Yanga waitisha mkutano wa Dharura.
Reviewed by Zero Degree
on
10/10/2016 09:47:00 AM
Rating: