Loading...

Azam yanasa kifaa toka Ghana.

MSHAMBULIAJI wa Medeama SC ya Ghana, Bernard Ofor.
MSHAMBULIAJI wa Medeama SC ya Ghana, Bernard Ofor yuko mbioni kujiunga na Azam FC ya Dar es Salaam baada ya makubaliano ya awali kukamilika.

Mchezaji huyo wa zamani wa New Edubiase United, aliondoka Ghana juzi na alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo kumalizana na washindi hao wa Ngao ya Jamii.

Akifanikiwa kusaini Azam FC, Ofori ataungana na wachezaji wengine wawili wa Medeama SC waliojiunga na Azam FC, ambao ni winga Enoch Atta Agyei na mshambuliaji Daniel Amoah.

Amoah amekwishajiunga na kikosi cha Azam FC kilicho chini ya kocha Mkuu, Mspaniola Zeben Hernandez wakati Agyei atajiunga na timu hiyo Januari atakapofikisha umri wa miaka 18.

Bado haijajulikana Azam FC itamtema nani ili kupata nafasi ya kuwasajili wachezaji hao kwani tayari imekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu.

Wachezaji hao ni mabeki Amoah Serge Wawa Pascal, kiungo Kipre Balou, Ya Thomas Lenardo, winga Bruce Kangwa na mshambuliaji Francisco Zekumbawira.

ZeroDegree.
Azam yanasa kifaa toka Ghana. Azam yanasa kifaa toka Ghana. Reviewed by Zero Degree on 11/09/2016 05:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.