George Lwandamina aingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya kocha bora Zambia.
WAKATI Ligi Kuu nchini Zambia ikielekea ukingoni, kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina, ameingizwa kwenye orodha ya wanaopigiwa chapuo kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka kocha bora wa Ligi Kuu ya Zambia msimu huu.
Mbali na Lwandamina, kocha wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Simba, Patrick Phiri, naye amewekwa kwenye orodha hiyo kutokana na juhudi zao walizozionyesha katika timu walizoziongoza.
Lwandamina, ambaye kwa sasa anasubiri kuanza kibarua chake rasmi na Yanga, ameingizwa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kazi kubwa aliyoifanya akiwa na Zesco United, ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ya nchini humo.
Kwa upande wake Phiri, ambaye ni moja ya makocha wapole lakini makini katika kazi yao, anakumbukwa jinsi alivyoinusuru na mkasi wa kushuka daraja timu ya Nakambala Leopards msimu uliopita.
Makocha wengine wanaopewa nafasi ya kuibuka kidedea katika patashika hiyo ni Mmisri Mohamed Fathy, ambaye licha ya kutimuliwa na timu yake ya Kabwe Warriors kutokana na kutofautiana na uongozi, kazi yake aliyoifanya inaonekana, huku pia akiwamo Tenant Chilumba.
Kwa mujibu wa mitandao ya nchini humo, makocha hao ndio ambao mmojawapo anapewa nafasi ya kuibuka kama kocha bora, huku pia Numba Mumbamba, ambaye amewahi kuwika zamani kama mchezaji, akipewa nafasi hiyo.

ZeroDegree.
George Lwandamina aingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya kocha bora Zambia.
Reviewed by Zero Degree
on
11/23/2016 10:35:00 AM
Rating: