Kauli ya Carrick yamtoa jasho kocha Jose Mourinho.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amepanga kumuongezea mkataba mpya kiungo Michael Carrick baada ya siku chache mchezaji huyo kusema kuwa huu unaweza ukawa msimu wake wa mwisho kuichezea timu hiyo.
Kiungo huyo aliyesajiliwa mwaka 2006 akitokea Tottenham Hotspur kwa dau la paundi milioni 18.6 alisema ujio wa Paul Pogba ndani ya timu hiyo kutaifanya nafasi yake ya kucheza kuwa ndogo.
Baada ya kauli hiyo, Mourinho amesema, “Michael ana miaka 35. Ni jambo baya sana kufahamu kwamba muda si rafiki wa mtu yeyote. Ni mchezaji mzuri ajabu na inatia huruma, mara nyingi nimekuwa nikimpenda sana, lakini badala ya kuwa meneja wake wakati alipokuwa na umri wa miaka 25 nimekuja kuwa meneja wake wkati ana miaka 35. Tunamaelewano mazuri naye. Tunatambua ni wakati gani tunaweza kucheza vema. Tunajua ni wakati gani yuko tayari na ni wakati gani apate mapumziko. Bado niko na Michael Carric na ikiwezekana hata msimu mmoja zaidi.
Kocha huyo ameongeza, “tumekuwa na dirisha la usajili na miezi mingine minne ya kazi,” alisema. “tunawachezaji wengi chipukizi na wengi wenye umri mkubwa na wazoe, hivyo tunahitaji kufanya kazi nyingi. Lakini kama ukijaribu kuangalia mechi tulizocheza dhidi ya Burnley, Stoke na Arsenal, kama ungekuwa na point 6 zote ambazo tulistahili, tazama ni wapi tungekuwa. Kama tutaendelea kucheza kama tunavyocheza sasa, tutakuwa salama. Ninahitaji timu ambayo itakuja hapa na kucheza vizuri zaidi yetu na kutufunga sisi. Ndipo unapoweza kurudi nyumbani na kusema hawa watu walikua na kiwango kikubwa zaidi yetu. Lakini kwa mchezo wa jumamosi, nilienda nyumbani nikijisemea katika mawazo yangu kwamba nimepoteza mchezo.

ZeroDegree.
Kauli ya Carrick yamtoa jasho kocha Jose Mourinho.
Reviewed by Zero Degree
on
11/21/2016 12:57:00 PM
Rating: