Klabu ya Azam yaachana na mchezaji mwingine wa pili kutoka nchini Ivory Coast.
Gonazo Bi Ya Thomas Renardo. |
Mapema mwezi huu, Azam FC iliwasaini washambuliaji Samuel Afful, Daniel Atta Agyei na Yahaya Mohammed wote kutoka Ghana.
Na ili kubaki na wachezajin saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni, Azam imewatema Waivory Coast wote, beki Serge Wawa, kiungo Kipre Michael Balou na mshambuliaji Renardo walioingia timu hiyo kwa wakati tofauti.
Gonazo Bi Ya Thomas Renardo (kushoto) aliyesajiliwa mwanzoni msimu huu Azam FC ameachwa baada ya kusajiliwa Waghana watatu. |
Balou alitangulia mwaka 2011 pamoja na pacha wake, Kipre Herman Tchetche ambaye mwanzoni mwa msimu alihamia Oman alikokwenda kujiunga na klabu ya Al Suwaiq, wakati Wawa alifuatia mwaka 2014, wakati Renaldo alisajiliwa Julai mwaka huu.
Afful, Agyei na Mohammed wanafanya idadi ya wachezaji wa Ghana kufika wane, baada ya beki Daniel Amoah aliyesajiliwa Agosti.
Hao wanaungana na kiungo Jean Baptiste Mugiraneza kutoka Rwanda na Wazimbabwe wawli, winga Bruce Kangwa na mshambuliaji Francesco Zekumbawira kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.
Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki mbili hadi Desemba 3 mwaka huu, kitakapoanza mazoezi ya kwanza kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na kombe la Shirikisho Afrika.
ZeroDegree.
Klabu ya Azam yaachana na mchezaji mwingine wa pili kutoka nchini Ivory Coast.
Reviewed by Zero Degree
on
11/28/2016 06:05:00 PM
Rating: