Kocha Ancelotti ataja warithi wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Soka kwa sasa lipo chini ya ulinzi wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi na wameishika dunia katika kila idara kuanzia tuzo hadi mikataba na makampuni ya biashara pamoja na malipo makubwa ya mishahara.
Kwa uwezo walioonesha nyota hawa ndani ya miaka 10 hakika kama rekodi itasalimika kuvunjwa basi huenda rekodi hiyo ikadumu milele.
Mtaalamu huyo wa ufundi raia wa Italia ameacha maswali mengi kwa wapenda soka kiasi cha kuzua mjadala mitandaoni kwa kurejea nyuma ambapo kocha huyo aliwahi kushutumiwa kuwa hana maelewano mazuri na nyota wa Wales Gareth Bale wakati akiifundisha Madrid.
Bosi wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ambaye amewahi kuinoa Real Madrid amewataja wachezaji wawili ambao huenda wakarithi mikoba ya mafanikio ya nguli hao wa soka kwa kizazi hiki.
Akiongea na mtandao wa Tuttosport, amewataja nyota wa Juventus Paul Dybala kuwa anauwezo wa kufanya makubwa ndani ya miaka 10 ijayo.
Mtaalamu huyo wa ufundi raia wa Italia ameacha maswali mengi kwa wapenda soka kiasi cha kuzua mjadala mitandaoni kwa kurejea nyuma ambapo kocha huyo aliwahi kushutumiwa kuwa hana maelewano mazuri na nyota wa Wales Gareth Bale wakati akiifundisha Madrid.
Neymar ndiye mchezaji wa pili kutajwa na Ancelotti kuwa ni mrithi mzuri wa Ronaldo na Messi katika kuendeleza ufalme wao waliojitengenezea katika kila idara inayohusu soka.
Siku za hivi karibuni makocha wamekuwa wakitoa misimamo yao juu ya nyota ambao wanaweza kuvaa viatu vya Messi na Ronaldo ambapo Pep Guardiola yeye alimtaja Kevin De Bruyne kama mchezaji bora baada ya Messi.
ZeroDegree.
Kocha Ancelotti ataja warithi wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Reviewed by Zero Degree
on
11/10/2016 02:44:00 PM
Rating: