Sababu tano zilizompa ushindi Donald Trump.
DONALD Trump alizima matarajio ya wengi kuhusiana na ushiriki wake katika mbio za urais wa Marekani tangu kuanza kwa kampeni takribani mwaka mmoja uliopita, baada ya kuibuka mshindi wa nafasi hiyo huku sababu tano zikitajwa kuwa ndiyo siri ya mafanikio yake.
Baada ya upigaji kura kufanyika juzi na kura kuhesabiwa, matokeo yalianza kutoka. Majimbo yaliyoaminika kuwa ngome ya Clinton yakaanza kuangukia kwa Trump moja baada ya jingine, yakiwamo ya Ohio, Florida na North Carolina.
Matokeo hayo miongoni mwa majimbo muhimu yakamuacha Clinton katika wakati mgumu.
Kete ya mwisho iliyokuwa ikitegemewa kwa kiasi kikubwa na Democrat ni nguvu ya Clinton katika eneo la magharibi ya kati.
Hilo ni eneo lenye majimbo ambayo kwa miongo kadhaa sasa yamekuwa yakiunga mkono wagombea wa Democrat, chanzo kimojawapo kikiwa ni ukweli kwamba ndimo kwenye uungwaji mkono mkubwa wa Wamarekani weusi na wazungu wa tabaka la wavuja jasho.
Wazungu hao wa tabaka la chini, hasa wale wasio na elimu ya chuo – wanawake kwa wanaume – walikihama chama cha Democrats kwa makundiu.
Wapiga kura wa maeneo ya vijijini walijitokeza kwa wingi, wakiwa miongoni mwa Wamarekani wanaomini kuwa walitengwa na mamlaka na kuachwa nyuma na wasomi wa mwambao na hivyo wakaamua kupaza sauti zao zisikike.
Wakati maeneo kama Virginia na Colorado yakimpa ushindi Clinton, Wisconsin liliangukia kwa Trump – na hapo matumaini ya ushindi wa Clinton yakazidi kupotea.
Kwa matokeo hayo, Clinton anaweza kubaki akijivunia ushindi katika maeneo kama California na New York, lakini akapoteza katika majimbo matata kama Utah.
Wimbi la Trump likamzoa Clinton katika maeneo aliyoamini kuwa ni ngome kwake. Na hiyo ikawa ni siri mojawapo ya safari ya Trump kuelekea Ikulu ya Marekani, maarufu kama ‘White House’.
2. MAPIGO DHIDI YA KASHFA
Trump aliamua kupambana na kituo cha televisheni cha Fox News na hasa mtangazaji wake maarufu, Megyn Kelly.
Alimjia juu mtangazaji huyo baada ya kuulizwa kuhusu ‘vituko’ alivyowahi kumfanyia kinara wa mashindano ya urembo Hispania.
Aliomba radhi kwa hisia kali juu ya picha ya ya siri ya video iliyovujishwa ikimhusisha na masuala ya mapenzi na warembo mbalimbali.
Baada ya hapo, Trump alishiriki midahalo mitatu ya wagombea urais ambako kote hakuonekana kufanya vizuri.
Hata hivyo, mambo yote hayo hayakumrudisha nyuma Trump.
Wakati akiendelea kuonekana akiporomoka katika matokeo ya kura mbalimbali za maoni, baada uungwaji mkono wake kwa wapiga kura uliendelea kuwa juu – hatimaye akaibuka mshindi na kushangaza wengi.
Inaelezwa kwua labda, mfululizo wa matukio kadhaa tata kuhusiana na nyendo za Trump yaliibuka kwa kasi kiasi kwamba hakukuwa na yeyote aliyekuwa na muda wa kuyafuatilia kiundani. Labda haiba ya Trump na ahadi zake vilikuwa na mvuto zaidi kiasi cha kufunika kashfa zilizoibuliwa dhidi yake.
3. KUJITENGA NA KINA BUSH
Licha ya Trump kupambana na Democrats, alikuwa akipambana pia na baadhi ya makada wa chama chake cha Republican. Hatimaye waliokuwa washindani wake katika mbio za kuteuliwa kugombea urais ndani ya Republican, wakiwamo Marco Rubio, Ted Cruz, Chris Christie na Ben Carson, hatimaye walikubali yaishe na kukubalianba naye. Wengine alibaki nao mbali, wakiwamo Jeb Bush na gavana wa Ohio, John Kasich.
Na hata makada muhimu wa ndani ya chama, wakiwamo Spika Paul Ryan, Trump hakuwategemea na wala hakuhitaji msaada wao. Kwa sababu hiyo, inaelezwa kuwa ushindi wake umechangiwa na kule kuonekana kuwa amejitenga dhidi ya makada hao.
Inaelezwa zaidi kuwa kitendo cha Trump kuonyesha kuwa hawategemei makada wa chama chake kimemuinua kwa kuthibitisha kuwa ni mtu mwenye fikra huru na sifa hiyo ni muhimu kwa umma wa Wamarekani.
4. KASHFA ‘EMAILS’ ZA CLINTON
Sababu nyingine inayotajwa kuwa siri ya ushindi wa Trump ni kuibuka upya kwa tuhuma za barua pepe (emails) binafsi za Clinton siku chache kabla ya uchaguzi. Sakata hilo linatajwa kumpunguzia kura Clinton na kumnufaisha Trump.
Awali, tuhuma kwamba Clinton alikiuka utaratibu wa kutumia ‘emails’ binafsi akiwa madarakani katika Serikali ya Rais Barack Obama halikuonekana kuwa na athari, lakini likapata nguvu baada ya Mkurugenzi wa FBI, James Comey, kutangaza kwamba wanachunguza upya suala hilo.
Licha ya FBI kueleza siku chache kabla ya kupiga kura kuwa wamebaini Clinton hakukosea popote, lakini inaelezwa kuwa tayari jambo hilo lilishamuathiri baada ya uungwaji mkono wake kupungua kwa kiasi kikubwa huku Trump akiimarika maradufu.
5. UNGANGARI WA TRUMP
Licha ya awali kuonekana kuwa si tishio, lakini Trump alionekana kuwa imara na kujua anachokifanya, muda wote akisimamia kile anachokiamini katika kujikubalisha kwa wapiga kura.
Inaelezwa kuwa alitumia muda mwingi katika kusaka kura kuliko kufuatilia matokeo ya kura za maoni. Alisafiri kwenda katika majimbo kama Wisconsin na Michigan ambayo wachambuzi wa amsuala ya siasa walisema hayatafikika.
Alifanya mikutano mikubwa ya hadhara badala ya kujieklekeza katika kuomba kura ‘nyumba kwa nyumba’. Hakuwa na hotuba ‘tamu’za kusisimua, lakini alivutia wengi kwa mismamo yake kulinganisha na kampeni za Clinton zilizohusisha matumizi makubwa ya fedha.
Mwishowe, Trump akaibuka mshindi na sasa safari yake ya kuingia Ikulu imetimia.
WALICHOSEMA TRUMP, CLINTON
Akihutubia maelfu ya wafuasi wa chama chake jijini New York baada ya kuibuka mshindi, Trump alisema atakuwa “Rais wa Wamarekani wote".
“Sasa ni wakati wa kuponya majeraha ya mgawanyiko. Nasema kwa wana Democrat na Republican, kwamba ni wakati wa kuungana na kuwa kitu kimoja,” alisema na kuongeza:
“Naahidi kuwa Rais wa Wamarekani wote…wanaume na wanawake waliosahauliwa nchini mwetu hawatasahauliwa tena.”
Akizungumza jana, Clinton alikubali kushindwa katika jaribio lake la kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Marekani na kumpongeza Trump.
Akimzungumzia Clinton, Trump alisema: “Ametupongeza…namimi nampongeza na familia yake kwa kampeni iliyokuwa na ushindani mkali.”
Trump aliyekuwa akiwania urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, aliwashangaza wengi, baada ya kupata kura 279 za kiti cha urais dhidi ya 218 za mpinzani wake, Hillary Clinton wa chama tawala cha Democrats.
Kura za kutosha kutoka kwa wazungu wasio na elimu ya kiwango cha chuo; namna alivyojibu mapigo kwa kashfa zilizoibuliwa dhidi yake ikiwamo ya kuhusishwa na mrembo wa Kihispaniola katika mahojiano na mtangazaji wa televisheni ya Fox News, Megyn Kelly, na kujitenga kwake na makada wazoefu wa chama chake cha Republican akiwamo Spika Paul Ryan, ni miongoni mwa sababu tano zinazotajwa kuwa ndizo zilizombeba Trump, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa uchambuzi wa vyanzo mbalimbali ikiwamo Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC.
Nyingine zinatajwa kuwa ni uwezo wa Trump kusimamia kile anachokiamini kwa kuendelea na mikutano ya hadhara ya kampeni hata katika maeneo yaliyodhaniwa kuwa asingekanyaga na sababu kubwa ya tano, inatajwa kuwa ni sakata la barua pepe binafsi za hasimu wake, Clinton, ambalo lilipata nguvu siku chache kabla ya uchaguzi kutokana na taarifa ya FBI iliyodai kuwa inafanya uchunguzi kubaini ukweli wa sakata hilo.
Awali, kabla ya uchaguzi juzi, matokeo ya kura nyingi za maoni yalikuwa yakimpa ushindi Clinton.
Ni watu wachache walioamini kwamba mwishowe atateuliwa kugombea, lakini akaitwaa nafasi hiyo.
Waliamini kwamba kamwe hatapanda katika kura za maoni, lakini akapanda.
Walisema hatashinda katika kura zozote za awali, lakini akashinda. Walisema hatateuliwa na chama chake cha Republican kuwa mgombea, lakini akateuliwa.
Mwishowe, walisema kwamba hakuna namna atakayoweza kupambana, achilia mbali kushinda, katika uchaguzi mkuu dhidi ya Clinton. Lakini sasa, Trump ndiye rais mteule wa Marekani.
1. KURA ZA WAZUNGU

ZeroDegree.
Sababu tano zilizompa ushindi Donald Trump.
Reviewed by Zero Degree
on
11/10/2016 01:40:00 PM
Rating: