Loading...

Lionel Messi agoma kusaini mkataba mpya Catalunya.

HALI si shwari katika klabu ya Barcelona na hiyo ni baada ya kuripotiwa kuwa staa wao Lionel Messi amegomea mpango wa kusaini mkataba mpya.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka Hispania, juhudi za viongozi wa Barca kumpa mkataba mpya mkali wao huyo zimegonga ukuta.

“Kwa sasa Leo Messi ana mkataba utakaofikia tamati baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia za Urusi (mwaka 2018),” alisema Rais wa Barca, Josep Bartomeu.

“Hatujui kitakachotokea hapo baadaye lakini tutakuwa tukijaribu kumwambia kuwa ni mchezaji bora duniani na hapa ndipo panapomfaa kuishi.”

Gazeti la Marca la jijini Madrid limenyetisha kuwa Messi alifikia uamuzi huo wa kutoongeza mkataba mpya tangu Julai alipokuwa mapumzikoni na mkewe Antonella Roccuzzo, ambapo pia aliambatana na watoto wake, Thiago na Mateo.

Imeelezwa kuwa moja kati ya sababu kubwa zilizochangia Messi kutaka kuondoka Catalunya, ni kashfa ya ukwepaji kodi ambayo kwa kiasi kikubwa ilimnyima raha.

Kwa upande wao, mabosi wa Barca hawaonekani kukata tamaa na wanaamini nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 atamwaga wino siku chache zijazo.

Hivi karibuni, Rais wa Barca, Josep Bartomeu, amewapa mikataba mipya mastaa Sergio Busquets, Neymar na Javier Mascherano.

Mbali na Messi, bado Barca wanahaha kurefusha mikataba ya Ivan Rakitic, Luis Suarez, Andres Iniesta na Marc-Andre Ter Stegen.

Mwezi uliopita, Bartomeu aliwaambia waandishi wa habari kuwa hana shaka kuwa Messi ataendelea kukipiga Camp Nou kwa miaka mingi ijayo, lakini sasa mambo yanaonekana kuharibika.

Kwa sasa Messi yupo na Mascherano kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina na mwezi uliopita staa mwenzake huyo alisaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Catalunya.

Kwa miaka kadhaa sasa, klabu za Paris Saint-Germain na Manchester City zimekuwa zikitajwa kuiwania saini ya staa huyo na huenda taarifa hii ikawa njema kwao.

ZeroDegree.
Lionel Messi agoma kusaini mkataba mpya Catalunya. Lionel Messi agoma kusaini mkataba mpya Catalunya. Reviewed by Zero Degree on 11/16/2016 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.