Loading...

Simba waanza timua timua.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope amesema kuwa mlango upo wazi kwa mchezaji anayetaka kuondoka na kamwe hawawezi kumzuia.

Akizungumza jana, Poppe alisema kuwa uongozi wa Simba na wanachama wamechoshwa na sarakasi zinazoendelea huku baadhi ya wachezaji wake wakidai kutaka kuondoka katika klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi na kutimkia kwa mahasimu wao.

Wachezaji ambao wanataja kwenda kusaka malisho nje ya Simba na Ibrahim Ajibu, Mohamed Hussein ‘Thabalal’ na Jonas Mkude. Hata hivyo, Poppe alisema jana kuwa wachezaji hao bado ni mali halali ya Simba na kwamba mikataba yao inamalizika mwakani.

“Mchezaji yeyote katika Simba anacheza kwa ridhaa yake na mapenzi yake mwenyewe, mchezaji yeyote ana hiyari ya kuondoka na kwenda kucheza timu yoyote ndani ya nchi au nje. “Haya mambo ya kupeana presha mara wanaenda Yanga mara Azam wakitaka waende tu, wasituletee vurugu, kwani hata kipindi cha miezi sita kuzungumza na haina maana kama kabakiza miezi sita lazima tuzungumze.

“Ni utaratibu tu, kama amebakiza miezi sita timu nyingine yoyote inaweza kuzungumza naye, sisi hatukatai mchezaji kuzungumza na timu nyingine, lakini wasubiri wabakize miezi sita, kama kuna timu zimeshaanza kufanya nao mazungumzo ni makosa na haya makosa yanalelewa na TFF na kamati zake. “Kikao cha Singano ambacho mwenyekiti ni Sinamtwa, Singano aliulizwa kwenye kikao kile alifuatwa na Yanga na Azam, na alikuwa na mwaka mmoja mbele lakini hakuna aliyechukuliwa hatua, vurugu zote zinalelewa na TFF.

Kauli ya Pope imekuja ikiwa ni siku chache kukiwa na taarifa kuwa baadhi ya wachezaji huenda wakaipa mkono Simba na kujiunga na wapinzani wao hususani Yanga au Azam.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa kuna mgomo baridi ndani ya klabu hiyo ambayo ilimaliza kwa kipigo mfululizo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa kwanza huku ikidaiwa kuwa wachezaji hao wamekuwa wakidai malimbikizo yao ya mshahara na posho zao mbalimbali.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemela akizungumzia suala hilo la ukata alisema, “Posho tumekuwa tukitoa Sh 400,000 kila mechi wanayoshinda, na pia mishahara yao tunawapatia bila tabu, sijui haya mambo yanatokea wapi, nadhani ni wapinzani wetu ndio wanaopandikiza vitu hivi.”

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Simba waanza timua timua. Simba waanza timua timua. Reviewed by Zero Degree on 11/16/2016 12:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.