Messi atajwa kuwa chanzo cha mashabiki wa soka Ureno kumchukia Ronaldo.
Uwepo wa Lionel Messi katika mchezo wa soka sio tu unaweza kuwa unamfanya Cristiano Ronaldo kushindwa kushinda kila taji ambalo anawania lakini pia hata kuwagawa mashabiki wa mchezo huo maarufu duniani hadi katika nchi ambayo ndiyo kwao na Ronaldo ya Ureno.
- Kauli ya Rais wa Barcelona baada ya kuenea kwa tetesi za Messi kugomea mkataba mpya.
- Messi awaliza mashabiki wa soka nchini Argentina.
- Lionel Messi agoma kusaini mkataba mpya Catalunya.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno, Paulo Futre amesema licha ya Ronaldo kupendwa na mashabiki wengi duniani lakini hali ni tofauti kwao Ureno kwa baadhi ya mashabiki kutokumpenda na hata kufikia hatua ya kutaka Messi ashinde tuzo ya Ballon d’Or 2016.
Alisema licha ya Ronaldo kuwa ameonyesha uwezo mkubwa na kushinda mataji makubwa kwa mwaka huu lakini bado mashabiki wa Ureno hawataki kukubali kuwa staa huyo ana uwezo kuliko Messi na wao wameshikilia msimamo wa kutaka Messi kuonekana bora zaidi ya Ronaldo.
“Cristiano ni Mreno, ameshafanya kila kitu, ni msindi wa kombe la Ulaya, lakini ana maadui wengi kwa jinsi tu alivyo. Ni muwazi na anatengeneza maadui wengi katika nchi yake,
“Kuna muda watu wanaimba ‘Messi, Messi, Messi’ nje ya hoteli ambayo inakuwa timu ya taifa ya Ureno. Aibu gani hii, bila shaka kuna watu Ureno wanataka Messi ashinde Ballon d’Or, hivi ndivyo walivyo Wareno,” alisema Futre.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno, Paulo Futre. |
“Cristiano ni Mreno, ameshafanya kila kitu, ni msindi wa kombe la Ulaya, lakini ana maadui wengi kwa jinsi tu alivyo. Ni muwazi na anatengeneza maadui wengi katika nchi yake,
“Kuna muda watu wanaimba ‘Messi, Messi, Messi’ nje ya hoteli ambayo inakuwa timu ya taifa ya Ureno. Aibu gani hii, bila shaka kuna watu Ureno wanataka Messi ashinde Ballon d’Or, hivi ndivyo walivyo Wareno,” alisema Futre.
ZeroDegree.
Messi atajwa kuwa chanzo cha mashabiki wa soka Ureno kumchukia Ronaldo.
Reviewed by Zero Degree
on
11/24/2016 12:35:00 PM
Rating: