Loading...

NATO yampa onyo Donald Trump.

NATO Secretary General Jens Stoltennburg.
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltennburg amemuonya rais mteule wa Marekani Donald Trump dhidi ya kufanya maamuzi ya kipekee, akisema kuwa sio chaguo la muungano wa Ulaya ama hata Marekani.

Amesema kuwa mataifa ya magharibi yalikabiliwa na changomoto yake kuu ya kiusalama.

Wakati wa kampeni zake za uchaguzi bwana Trump aliutaja muungano huo wa kijeshi wa mataifa ya Magahribi kama uliopitwa na wakati.

Alisema kuwa Marekani itafikiri mara mbili kumsaidia mwanachama yeyote wa muungano huo ambaye ameshambuliwa iwapo hajalipa kodi yake ya uanachama.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Akiandika katika gazeti moja la Uingereza Observer,bw, Stoltenberg alikiri kuhusu umuhimu wa baadhi ya wanachama kulipa kodi ya juu kwa kuwa Marekani inagharamikia asilimia 70 ya matumizi ya muungano huo.

Lakini ameongezea kuwa viongozi wa Marekani wamekuwa wakitambua kwamba wana washirika muhimu barani Ulaya kupitia usalama na udhabiti walio nao.

Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
NATO yampa onyo Donald Trump. NATO yampa onyo Donald Trump. Reviewed by Zero Degree on 11/13/2016 01:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.