Laudit Mavugo atetewa na jopo la makocha.
WAKATI mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ukiwa umemalizika na timu mbalimbali kuanza mikakati ya usajili wa dirisha dogo, baadhi ya makocha wamewaambia Simba watakuwa wamefanya kosa kubwa kama lile walilolifanya kwa Amis Tambwe, endapo wataamua kumtema Laudit Mavugo.
Tayari mashabiki wameanza kupiga kelele juu ya kuhitaji straika huyo atemwe ili apishe wengine kuingia, huku akitajwa Emmanuel Okwi na Kipre Tchetche, ambao huenda wakarejea kucheza soka la Tanzania katika kikosi cha Simba.
Mashabiki hao wa Simba wanadai kuwa mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika, Mavugo hajaonyesha lolote la maana kama walivyokuwa wametarajia na wengine kwenda mbali zaidi wakitaka afungashiwe kila kilicho chake.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, baadhi ya makocha hao walisema Mavugo ni straika mzuri sana ambaye anatakiwa kuendelea kupewa muda na kwamba Simba wasije wakakurupuka kumtosa, kwani watakuja kumkumbuka.
Kocha wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Goran Kopunovic, ambaye wakati akikinoa kikosi hicho alipendekeza straika huyo asajiliwe, alisema analifuatilia sana soka la Tanzania na kwamba Mavugo bado hajazoeana na wenzake, kitu ambacho kinampa tabu.
“Ninachoona ni kwamba, bado upepo haujamwendea vizuri, inawezekana hajazoeana na wenzake vizuri, naamini akikaa sawa atawasaidia sana, kwani naujua uwezo wake ulivyo, wasithubutu kumtema,” alisema.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, alisema hana matatizo na straika wake huyo, kwani ana imani atakuja kuwa mzuri na kuwafunga midomo wanaomuona hafai kwa sasa.
“Mavugo amejiunga na timu dakika za mwishoni tukiwa katika maandalizi ya mwisho ya ligi, hivyo bado hajafahamu falsafa zangu, naamini siku za karibuni watu watamkubali,” alisema.
Alisema katika kipindi hiki cha mapumziko ana imani kwamba Mavugo atarudi kivingine na kuufanya mzunguko wa pili kuwa mzuri kwa Wwekundu hao wa Msimbazi.
“Naamini haya mapumziko ya siku kadhaa yatamfanya kurudi upya akijua wazi kuwa anatakiwa kuifanya Simba itwae ubingwa msimu huu, akishirikiana na wenzake, najua watu wataanza kumkubali,” alisema Omog.

ZeroDegree.
Laudit Mavugo atetewa na jopo la makocha.
Reviewed by Zero Degree
on
11/13/2016 01:45:00 PM
Rating: