Loading...

Simba yaweka mtego kila kona.

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, wameanza kusaka straika wawili wa kusaidiana na Laudit Mavugo, kwenye nchi mbalimbali ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Simba ilianza vyema ligi kuu na kuongoza kwa muda mrefu ikicheza mechi 13 bila kupoteza, ikishinda 11 na sare mbili lakini ghafla kibao kikageuka kwenye raundi mbili za mwisho na timu hiyo ikapoteza mechi mbili mfululizo, ikifungwa 1-0 African Lyon na kupokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons.

Kufanya vibaya kwenye michezo hiyo kumemfanya kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, kutangaza kufanya usajili kwenye maeneo mbalimbali ikwemo safu ya ushambuliaji na mlinda mlango.

Kauli hiyo ya Omog inawafanya mawakala mbalimbali kuanza kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo, huku vigogo nao wakihaha huku na huku kusaka nyota katika nafasi hizo.

Tayari Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Godfrey Nyange Kaburu pamoja na msemaji wa timu hiyo, Haji Manara, wapo nchini Zimbabwe na kikosi cha Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya Fifa ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa makini kuangalia nani anaweza kuwafaa kwa nafasi zilizotajwa na kocha.

Tayari mchezaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe, Rodreck Mutuma, anayekipiga katika klabu ya Dynamos Fc ameelezwa kuwa kwenye rada za Simba ambapo pia imeelezwa huenda Kaburu na Manara wakamuona kwa ajili ya mazungumzo.

Mbali na straika huyo kutoka Zimbabwe, Simba inasaka nyota kwenye nchi za Afrika Kusini, Rwanda, Uganda, Kenya na Malawi kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Wekundu hao wa Msimbazi wanasaka kipa atakayesaidiana na Vincent Angban, beki wa kati na washambuliaji ambao watasaidiana na Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib.

ZeroDegree.
Simba yaweka mtego kila kona. Simba yaweka mtego kila kona. Reviewed by Zero Degree on 11/14/2016 09:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.