Loading...

Stars yachezea kichapo cha goli 3 bila Zimbabwe.

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana ilipokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Zimbambwe katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa nchini humo.

Mchezo huo ambao uko katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), ungeipandisha viwango Stars kama ingeshinda, lakini kitendo cha kufungwa kinaweza kuzidi kuiporomosha zaidi, ambapo mwezi huu ilikuwa ya 159.

Zimbabwe waliandika bao la kwanza katika dakika ya tisa lililofungwa na Knowledge Musona baada ya mabeki wa Taifa Stars kushindwa kuzuia.

Dakika 53 tangu kuanza kwa mchezo huo, Zimbabwe waliongeza bao la pili kupitia kwa Rusike Mathew baada ya kucheza pasi kadhaa kuanzia pembeni ya uwanja hadi katikati kisha kupiga shuti kali lililojaa wavuni.

Bao la tatu la Zimbabwe lilipatikana katika dakika ya 56 likifungwa na Mushekwi baada ya mpira wa faulo uliopigwa kutoka upande wa kulia kupita moja kwa moja hadi wavuni.

Dakika ya 69 Stars ilifanya mabadiliko baada ya kumtoa Simon Msuva na kumuingiza Thomas Ulimwengu huku ikimtoa Yassin Mzamiru na kumuingiza Mohamed Ibrahim.

Kwa matokeo hayo, Zimbabwe imefanikiwa kulipa kisasa cha kufungwa mwaka juzi na Taifa Stars kwa bao 1-0 huku bao hilo la ushindi likiwekwa kimiani na John Bocco katika dakika ya 15.

ZeroDegree.
Stars yachezea kichapo cha goli 3 bila Zimbabwe. Stars yachezea kichapo cha goli 3 bila Zimbabwe. Reviewed by Zero Degree on 11/14/2016 10:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.