Loading...

Yanga waifunga Ruvu Shooting goli 2 - 1, ..wanasalia nafasi ya pili kwa tofauti ya point 2 toka kwa vinara.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara wana wajangwani Yanga, wamemaliza michezo ya mzunguko kwanza kwa ushindi dhidi ya Ruvu Shooting.

Yanga walipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa katika dimba la uhuru Jijini Dar es Salaam.

Ruvu Shooting ndio walianza kuzifumani nyavu za Yanga kwa bao la Abdulrahman Mussa kwenye dakika ya saba ya mchezo.

Winga wa Yanga Simon Msuva akaisawazishia timu yake bao hilo kwenye dakika ya 32, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga goli la pili na la ushindi katika dakika ya 56 kipindi cha pili.

Yanga wanasalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 33, huku wapinzani wao Simba wakiwa kileleni kwa alama 35.

Ligi kuu inasimama kwa muda na mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Desemba, mwaka huu.

ZeroDegree.
Yanga waifunga Ruvu Shooting goli 2 - 1, ..wanasalia nafasi ya pili kwa tofauti ya point 2 toka kwa vinara. Yanga waifunga Ruvu Shooting goli 2 - 1, ..wanasalia nafasi ya pili kwa tofauti ya point 2 toka kwa vinara. Reviewed by Zero Degree on 11/11/2016 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.