Loading...

Ahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu.

DEREVA Boniface Chuwa (29) mkazi wa Mwembetogwa, River Side, mkoani Morogoro, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kuwasafirisha wahamiaji haramu.

Hukumu hiyo ni ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani, ilitolewa na Hakimu Herieth Mwailolo.

Mwendesha mashitaka mwandamizi wa serikali, Mselei Mfinanga, ameieleza mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 22 mwaka huu, eneo la Mizani Mkuranga.

Alikamatwa akiwa na wahamiaji haramu 31 kutoka Ethiopia.

Amedai kuwa alikamatwa akiwa anaendesha gari aina ya Mitsubishi Canter, namba T 786 BBX, mali ya Jumanne Mohamed.

Mshitakiwa alikiri kosa.

Baada ya kupatikana na hatia hiyo, mahakama ilitoa adhabu hiyo au kulipa faini ya Sh milioni 20.

Alishindwa kulipa kiasi hicho hivyo amekwenda gerezani kutumikia kifungo hicho cha miaka 20.


ZeroDegree.
Ahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu. Ahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu. Reviewed by Zero Degree on 12/02/2016 01:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.