Loading...

Breaking News: Swansea City wamfungisha virago Kocha Bob Bradley baada ya kuitumikia klabu kwa siku 85.

Bob Bradley.
Baada ya mechi 11 tu na siku 85 katika wadhifa wake wa Ukocha akiwa na kikosi cha Swansea City ya Uingereza, Bob Bradley afukuzwa kazi.

Swansea City imetangaza jana siku ya Jumanne kwamba mmarekani amefukuzwa kazi baada ya kushinda mechi mbili tu za ligi kuu ya Uingereza tangu alipochukua nafasi ya Francesco Guidolin mwezi Oktoba.

Bob Bradley.
Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya wanaume Marekani aliingia katika nafasi ngumu wakati wa kuchukua nafasi ya utawala kama kocha wa klabu ya Swansea, hata hivyo, shinikizo kubwa kutoka kwa wafuasi na vyombo vya habari nchini Uingereza kuna uwezekano mkubwa imechangia kutimuliwa kwa Bradley.

Kabla ya kuchukua kibarua cha ukocha Swansea mwaka 2016, Bradley amewekuwa kocha wa klabu ya Ufaransa Le Havre, Kocha wa timu ya taifa ya wanaume Marekani na Timu ya taifa ya 
Misri ikiwa miongoni mwa nyingine.

Swansea sasa inashika naafasi ya pili kutoka mkiani mwa ligi kuu ya Uingereza wakati msimu unapokaribia hatua nusu ya mzunguko baada ya klabu kukubali magoli 41 ya ligi katika michezo 18 ya ligi.

ZeroDegree.
Breaking News: Swansea City wamfungisha virago Kocha Bob Bradley baada ya kuitumikia klabu kwa siku 85. Breaking News: Swansea City wamfungisha virago Kocha Bob Bradley baada ya kuitumikia klabu kwa siku 85. Reviewed by Zero Degree on 12/28/2016 12:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.